Kutoka Tabora
Na. Cosmas M. Njingo. GAIRO DC
Maafisa Elimu Mkoa na Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri zote Nchini, wametakiwa kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu sambamba na kukamilika kwa wakati miradi hiyo kwa lengo la kuepuka hoja za ukaguzi.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu (Elimu) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde wakati akifungua kikao kazi cha kuwajengea Uwezo Maafisa hao kuhusu Usalama wa Mazingira na Jamii katika kutekeleza miradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (Tanzania Secondary Education Quality Improvement Project - SEQUIP) kilichofanyika Agosti 15, 2022 Mkoani Tabora.
“Wajibu wenu kama viongozi ni kuhakikisha mnaenda kusimamia kikamilifu utekelezaji wa ujezi wa Miradi ya kuboresha miundombinu ya Elimu, hii itasaidia kupunguza hoja mbalimbali za ukaguzi zinazohusu utekelezaji wa miradi hiyo katika ngazi ya Serikali za Mitaa, husani kwa shule za Sekondari chini ya Mradi wa SEGUIP” Alisma Naibu Katibu Mkuu huyo.
Dkt. Msonde akafafanua kwamba Serikali inaendelea kujenga na boresha miundombinu ya elimu kwa fedha za mradi wa SEQUIP lengo kubwa ni kuboresha elimu ya sekondari, kuongeza fursa ya upatikanaji wa elimu kwa wananfuzni wanaohitimu Elimu ya Msingi na kupata ufaulu unawawezesha kujiunga na kidato cha kwanza, pamoja na kupunguza vikwazo vinavyosababisha wanafunzi kuacha shule.
“Serikali inaendelea kuwezesha mradi wa SEQUIP ili kuhakikisha miundombinu yote ya shule za sekondari inaboreshwa, lengo la Serikali yetu ni kufungua fursa kwa watoto wetu wapate elimu ya sekondari katika mazingira rafiki, sambamba na kuwaondolea vikwazo vina kuwasaidia wanafunzi kumaliza elimu bora ya sekondari na kupunguza changamoto za upatikanaji wa elimu nchini”. Alisema
Kwa upande mwingine Dkt. Msonde amewataka Maafisa hao kuto kujiingiza katika migogoro ya ardhi inayoweza kusababisha matatizo ikiwepo kushindwa kuendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo, na kwamba ni muhimu kujikita kwenye kusimamia ujenzi ili iendane na thamani ya fedha iliyotolewa, pia kusimamia utekelezaji wa ujenzi uzingatie kwa kuzingatia muda uliowekwa ili ikamilike kwa wakati na kutoa fursa kwa Wanafunzi kuanza masaomo haraka.
“Ninyi ni wabobezi katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya elimu, tushirikiane sote kusimamia hii miradi iwe yenye tija katika Taifa letu. Lakini kikubwa zaidi miradi ikamilike ndani ya muda uliowekwa ili watoto wetu wapate fursa ya kunufaika na elimu bora” alifafanua Dkt. Msonde
Akitoa ufafanuzi kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu (Elimu) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde, Mkurugenzi Msaidizi Idara Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bi. Hadija Mcheka alisema, kikao hicho kimewakutanisha Maafisa elimu hao kwa lengo la kuwajengea uwezo wakasimamia miradi yao kwa weledi mkubwa ambapo mbada mbalimbali zilifundshwa.
“Ndg Naibu Katibu Mkuu Dkt. Msonde kikao hiki ni cha siku mbili, ambapo tunatarajia Maafisa Elimu hawa watapitishwa kwenye mada mbalimbli ambazo zitawasaidia kuwa na uwelewa wa pamoja katika kupanga, kusimamia na kutekeleza maelekezo ya Serikali hususani kwenye usimamizi wa Miradi ya maendeleo”, Alisema Bi. Mcheka.
Aidha alisema Maafisa hao watapata ujuzi wa kitaalam utakaowawezesha kupata mbinu kufahamu taratibu za usimamizi wa miradi na kupata nafasi ya kutoa maoni katika kufanikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi.
Akizungumza kwa niaba ya washirike wenzake Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Bw. Juma Kaponda aliipongeza Serikali kwa kuendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu, ambapo waliahidi kwenda kuisimamia na kutekeleza kwa vitendo kwa kuzingatia sheria, miongozo na taratibu zinazowataka ili kuhakikisha sekta elimu ina;eta matokeo chanya kwa Taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa