PICHANI: Waliokaa, ni Kaimu Katibu Tawala (W) Bi. Annamarry Mwasendwa (kati kati) akiwa na Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Dkt. Reuben Mfugale (kulia) pamoja na Kamanda TAKUKURU (W) Bi. Renalda Mangia (kushoto), waliosimama kutoka kulia ni Mtendaji wa Kata ya Leshata Ndg. Salum Dibega akionyesha cheti cha ushindi wa Nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa Viashiria vya Lishe kwenye kata yake, akifuatiwa na Mshindi wa Pili kutoka kata ya Nongwe Ndg. Ishungisa Bartholomeo Kezerrra na Mtendaji wa Kata ya Mandege Ndg. Felix Alphoce Hinju (wa mwisho kushoto).
Na. Cosmas Mathias Njingo, GAIRO DC
LISHEKaimu katibu Tawala Wilaya ya gairo Bi. Annamarry Mwasendwa amewataka Watendaji wa Kata kuweka mikakati madhumbuti ya kusimamia afua za Lishe na utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika maeneo yao, ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kwa watoto wadogo wa Wanafunzi kutokana na ukosefu wa Lishe Boara.
Ametoa kauli hiyo Julai 19.2022 wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Jabiri Omari Makame wakatai wa kikao na Watendaji wa Kata cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ngazi ya Kata kwa mwaka 2021/2022 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
“Tuhakikishe sisi Watendaji tunasimamia vizuri utekelezaji wa Mkataba wa Viashiria vya lishe kwa kuweka mpango mkakati utakao tuwezesha kufikia malengo na kupanda kutoka asilimia 72 za matokeo ya utekelezaji mwaka 2021/2022 kufikia angalau asilimia zaidi ya 80 kwa mwaka ujao wa 2022/2023”. Alisema Kaimu Katibu Tawala Huyo.
Bi. Mwasendwa akawasisitiza Watendaji hao kuhakikisha wanashiriki kwenye kampeni mbalimbali za kutoa elimu kwa umma mara kwa mara, sambamba na kuendesha vikao vya Kamati za Lishe ngazi ya kata na vijiji kwa ajili ya kufikisha elimu kwa wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa Lishe kwa watoto sambamba na kusisitiza Wazazi na Walezi kuhudhuria kliniki kwa ajili ya kupata maelekezo muhimu yanayo husu Lishe.
Kaimu katibu Tawala (W) Bi. Annamarry Mwasedwa akizungumza na Watendaji wa Kata (hawapo pichani) kwenye kikao cha taarifa za Utekelezaji wa Mkataba wa Viashiria vya Lishe, kilichofanyika Julai 19/2022 katika ukumbi wa Halmashauri)
“Lengo letu hatutamani kuona Gairo inakuwa na watoto wenye vichwa vikubwa na wenye utapia mlo kwa kukosa Lishe sahihi kuanzi umri wa miezi sita hadi miaka 17 kwa vijana ambao tayari wapo mashuleni katika ngazi za Msingi na Sekondari, hivyo jukumu letu kubwa ni kuhakikishatunafanya vikao vya kutosha na kuelezea maswla aya Lishe pia kuwasisitiza Wazazi na Walenzi wahudhurie Kliniki ”. Alisema.
Kuhusu chakula mashuleni, Kaimu Katawala Bi. Mwasendwa, akashauri Watendaji hao kuendelea kuwahamsisha Wananchi kuchangia upatikanaji wa chakula cha kutosha mshuleni ili kuwazesha wanafunzi kupata chakula cha mchana lengo ni kupunguza utapiamlo ma kuondoa matokeo mabovu mashuleni sambamba na kuunda sharia ndogo za kuwabana wazazi wanaokwepa kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao shuleni.
Baadhi ya Watendaji wa Kata wakihudhuria kikao cha taarifa za utekelezaji wa Mkataba wa Viashiria vya Lishe cha julai 19,2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
“Kawekeni sheria ndogo za kuwabana wazazi na walezi wanaosumbua au kugoma kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao Mashuleni lengo ni kuhakikisha kila mazazi na kila mlezi anamwezesha mtoto wake kupata chakula shuleni ili kuimarisha lishe ma tuomdokane na hali ya utapia mlo kwa watoto wetu.” Alisisitiza.
Sambamba na hayo Bi Mwasendwa alisema ni muhimu kwa Watendaji hao kuelekkeza wanawake wajawazito waweke utaratibu wa kuhudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito, na kwa wale wanaofika wakati wa kujifungua lazima waende kupata huduma za uzazi salama kwenye vituo cya kutolea huduma za afya mapema badala ya kujifungulia nyumbani, halii hii itasaidia kuondokana na matatizo ya watoto wenye vichwa vikubwa.
Baadhi ya Watendaji wa Kata wakihudhuria kikao cha taarifa za utekelezaji wa Mkataba wa Viashiria vya Lishe cha julai 19,2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Dkt. Godbless Luhunga akimkaribisha Kaimu katibu Tawala Bi. Annamarry Mwasendwa kufungua kikao hivho kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mhe. Jabiri Omari Makame alisema Halmashauri itaendelea kuhakikisha inatenga bajeti kwa ajili ya kuwezesha shughuli za lishe na utekelezaji wa Mkataba wa Voashiria vya Lishe kutekelezeka kwa kuzingatia maelekezo na miongozo iliyotolewa na Serikali.
“Wajibu wetu kama Halmashauri ni kuhakikisha tunaendelea kutenga majeti kwatika kila mwaka ili kuhakikisha tunafanikisha utekelezaji wa malengo yaliyowekwa katika Mkataba wa Viashiria vya Lishe”, alisema Dkt. Luhunga
Awali akiwasilisha taarifa ya matokeo ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa mwaka 2021/2022 ngazi ya Kata, Mratibu wa Lishe Wilaya Bi. Loveness Achimpota alisema utekelezaji wa Mkataba wa viashiria vya Lishe ulianza tangu mwaka 2018 kwa agizo la Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Serikali ya awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Dakta John Pombe Magufuli.
Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya Dakta. Reuben Mfugale akifafanua jambo kwenye kikao cha kupitia taarifa za Utekelezaji wa matokeo ya Mkataba wa Viashiria vya Lishe julai 19.2022 katika ukumbi wa Halmashauri.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba huu ulitolewa agizo mwaka 2017 na aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya awamu ya tano Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye kwa sasa ndiye Rais wa Serikali ya awamu ya Sita, ambapo utekelezaji wake ulianza mwezi Januari 2018.” Alieleza.
Mratibu wa Lishe Halmashauri ya Wilaya Bi. Loveness Achimpota akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mkataba wa Viashiria vya Lishe katika kikao na Watendaji wa Kata Julai 19.2022
Katika kikao hicho kata tatu za Leshata, Nongwe na Mandege zilipongezwa kwa kupewa vyeti vya Kutambua mchango wao mkubwa na kufanya vizuri katika utekelezahi wa Viashiria vya Lishe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa