Kikao hicho kilihusisha Timu ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Wakuu wa Taasisi zote zilizopokatika Wilaya ya Gairo, Mkurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri, Maafisa Tarafa wa Tarafa mbili za Wilaya ya Gairo, Watendaji wa Kata zilizopo katika Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo na Wenyeviti wa Vitongoji vya Mamlaka ya Mji Mdogo.
Akifungua kikao hicho, Mh. Mkuu wa Wilaya ya Gairo alianza kwa kutoa pongezi kwa kufanya na kumaliza salama uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais uliofanyika tarehe 28/10/2020 na kusisitiza kuwa kazi zinatakiwa kuendelea pia mabadiliko ya awamu ya kwanza ya Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuingia awamu ya pili na kuasa kwamba lazima mabadiliko yaendane na kasi ya Mh. Rais.
Aliongeza kwa kusema ni lazima kujipanga upya na kuangalia changamoto na mafanikio ya awamu ya kwanza, aidha alisisitiza mambo yafuatayo:-
Mwisho aliwakaribisha wenyeviti wa Vitongoji kutoa pongezi, kero, changamoto na mafanikio toka kwa wananchi, na wakuu wa Taasisi na Mkurugenzi walizipokea changamoto na kero na kuahidi kuzifanyia kazi kadri inavyowezekana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa