Na. Cosmas Mathias Njingo.
GAIRO, Morogoro.
Nov. 01.2022
Kikundi cha Wanawake 15, cha wanufaika wa TASAF kitongoji cha Midindo kata ya Mandege kimezalisha kiasi cha Shilingi 1,269,000 (milioni moja laki mbili na elfu sitini na tisa kutokana na biashara ya kuuza mahindi kwa bei ya reja reja.
Wanakikundi wa Kikundi cha JITAHIDI, kitongoji cha Midindo, Kijiji cha Ikwamba, Kata ta Mandege katika picha ya pamoja, walipotembelewa na mwandishi wetu kujionea shughuli za kiuchumi zinazotekelezwa na kikundi hicho (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Wajumbe wa kikundi hicho wamesema katika msimu wa ujao wa kilimo wamepanga kulima ekari 4 za zao la mahindi na ekari 2 za zao la maharage ikiwa ni mkakati kabambe wa kukuza pato la kikundi na kuboresha maisha yao.
“Hizi pesa tulizopata tumapanga kulima ekari sita, kati ya hizo 4 za mahindi na 2 za maharage. Hii itatusaidia kukuza pato la kikundi chetu, na kutuwezesha kupata fedha za kujikimu ndani ya familia pamoja na kuimarisha uchumi wa mwanakikundi mmoja mmoja”. Alisema mmoja wa wana kikundi hao.
Moja ya stoo ya kuhifadhia mahindi ya kikundi cha Jitihada (PICHA NA: Cosmas Mathias NJingo)
Kikundi hiki cha Jitahidi kilianzishwa Januari 2.2022 kwa mtaji wa shilingi 200,000 (laki mbili). Kiasi hicho cha fedha kilipatikana kwa njia ya michango ya wanachama na baadaye kikazungushwa kwa njia ya kukopeshana fedha kiasi cha shilingi 10,000 (elfu kumi) huku riba ikiwa shilingi 2,000 hivyo marejesho yote kuwa shilingi 12,000 kwa kila mmoja kwa kila mwezi.
Viongozi wa Kikundi cha Jitahidi katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ikwamba Bw.Yosia Yolam (mwenye shati la rangi ya orenji) na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bw. Kashindye Severine Kassote.
Wakitoa maoni yao kwa Serikali wanakikundi hao wamemuomba Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuongeza jitihada na kiwango cha kuwezesha kiuchumi vikundi vya wanawake wanufaika wa TASAF ili kuwaongezea mitaji ya kuwasaidia kujikwamua na hali ya umskini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa