Wilaya ya Gairo Mkoa wa Morogoro, imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kimkoa Machi 8.2023.
Sherehe za Kilele cha maadhimisho hayo zimefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Gairo 'A' nakuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiongizwa na Wanawake Mkoa wa Morogoro.Mgeni Rasmi Mhe. Fatmwa Mwassa akiwakilishwa na Mkuunwa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli, amaewaasa wanawake wajasiliamali kuongeza ubunifu katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kutofautiana na wabunifu wengine na kuongeza tija katika ushindani wa soko.
Aidha Mhe. Nguli ameiomba jamii nzima ya wakazi wa Mkoa wa Morogoro kusimama kidete katika kupinga vitendo vya unyanyasaji wa watoto ikiwepo ulawiti, ubakaji na matukio mengine yanayovunja heshima ya mtoto.
Sherehe hizi awali zilitanguliwa na maandamano yaliyoongozwa na Brass Band kuanzia Viwanja vya Stand ya zamani maarufu Stand ya Shabiby Villa Pub hadi Viwanja vya Shule ya MsingiWanawake Mkoani Morogoro wametakiwa kuwa wabunifu wa miradi na bidhaa mbalimbali zenye mvuto wa hali ya juu ili kuleta utofauti na bidhaa za wabunifu wengine.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomelo Mhe. Judith Nguli akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kilichofanyika Machi 8.2023 Kimkoa katika Wilaya ya Gairo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa