Na. Cosmas M. Njingo.
Gairo Morogoro
Agosti.23.2022
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Sahili Geraluma Nyanzabala, amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatekeleza agizo la Serikali la kutenga 10% za mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya kuwezesha kiuchumi Vikundi vya uzalishaji mali vya Wanawake, Vinaja na Watu wenye Ulemavu.
Ametoa kauli hiyo Agosti 23, 2022 wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 Wilaya ya Gairo, na tarehe 24 Agosti 2022 kwenye makabidhiano ya Mwenge kati ya Wilaya ya Gairo na Kilosa yalofanyika kijiji cha Nhembo.
“Ndugu zangu Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kote Nchini, Serikali imeagiza kila Halmashauri ihakikishe inatenga 10% kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya kiuchumi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu”. Alisisitiza Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Makame, akikabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adamu Iddi mgoyi, alisema Mwenge huo ukiwa Wilayani Kilosa umekimbizwa umbali wa kilometa 179.5 katika kata 9 za Tarafa ya Gairo na miradi 6.
(Kiongozi wa Mbio za Mwnege wa Uhuru Kitaifa Ndg. Sahili Nyanzabala Geraluma akiaga viongozi na Wananchi wa Wilaya ya Gairo wakati wa makabidhiano ya mwenge huo kati ya Wilaya ya Kilosa na Gairo katika kijiji cha Nhembo Wilaya ya Kilosa)
“Mwenge wa Uhuru 2022, ukiwa Wilayani Gairo, ilikimbizwa katika maeneo mbalimbali umbali wa kilometa 179.5, ambapo uliona, kuzindua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi 6,yenye thamani ya Sh.Bilioni 1,198,476,916.72”. Alisema Mhe. Makame.
Agosti 24.2022 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabiri Omari Makame, alipokea Mwenge wa Uhuru Kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatuma Mwasa, ambaye aliupokea Kimkoa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamula.
(Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adamu Iddi mgoyi, akipokea Mwenge wa Uhuru 2022 kutika kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame)
Aidha ukamilishaji wa miradi hiyo, umechangiwa na fedha za michango kutoka Serikalini Kuu na wadau mbalimbali wa maendeleo. Ambapo Serikali Kuu imetoa kiasi cha Shilingi 856,423,771.05, Mchango wa Halmashauri Shilingi. 16, 377, 239.00, Watu Binafsi Shilingi 318,000,000 na Mchango wa Mwenge Shilingi 1,000,000, na kufanya jumla kuu ya Fedha za michango ywa mwenye kuwa shilingi 1,198,476,916.72.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 Kitaifa alikubali na kupitisha miradi yote iliyotembelewa na mbio na kupongeza Wanagairo kwa mapokezi mazuri na ushirkiano walioutoa wakati wa kukimbiza mwenge Wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa