Kuelekea Siku Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, amewataka Wanawake wanaofanya biashara ndogondogo wa wauzaji wa mazao kushiriki kikamilifu katika kuinua Maendeleo ya Wilaya kwa kuhakikisha wanalipa ushuru na tozo mbalimbali za Serikali bila kukwepa au kutorosha mapato ya Halmashauri.
Akizungumza na Wanawake Wachuuzi wa maharage katika gulio la Rubeho kata ya Rubeho. Mhe. Makame pamoja na kuwatia moyo wafanya biashara hao alisema swala la kulipa ushuru ni muhimu katika ukuaji wa uchumi na utekeleaji wa shughuli za miradi ya Maendeleo kwa Wananchi kwani tozo hizo ndio zinazotumika kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwepo shule, zahanati, maji na barabara kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.
Aidha aliwaambia wafanyabiashara hao Wanawake kuwa Serikali ipo kazini wakati wote kuwahudumia Wananchi wake pamoja na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili hivyo kila Mwananchi anawajibika kuwa mdau namba moja wa kutekeleza majukumu yake mahali alipo.
KAULI MBIU YA SIKU YA WANAWAKE āUbunifu na Mabadiliko ya Teknolojia, Chachu katika kuleta Usawa wa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
HakimilikiĀ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa