Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Agosti 15.2023.Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Gairo Mhe. Raheli Nyangasi, amemwagiza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmshauri hiyo pamoja Na Wakuu wa Divisheni za Elimu Awali, Msingi na Sekondari kuhakikisha shule zote zinatoa chakula cha mchana kwa Wanafunzi ili kuongeza bidi ya mahudhurio na kuinua ufaulu
Ametoa kauli hiyo Agasti 11.2023 katika hotuba yake ya ufunguzi wa Kikao cha Kawaida cha Baraza la Waheshimiwa Madiwani cha kujadili taarifa za Robo ya Nne kwa kipind cha Aprili Juni 2022/2023 kwenye ukumbi mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri.
“Ninakuagiza Mkurugenzi na Wataam wako wa divisheni husika, hili nalo mkalishughulikie. Tunataka kufikia Agosti 30.2023 kila shule iwe imeanza kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wote’. Aliagiza Mhe. Nyangasi.
Mwenyekiti huyo wa Halmashauri akabinisha kuwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vipo vya aina nyingi, nakuongezw kwamba hata kutowapatia Wanafunzi chakula cha mchana shuleni ni mojawapo ya vitendo vinavyoashiria ukatili kwao hali ambayo inadumaza ustawi wa maendeleo yao na kuondoka usiku.
“Kitendo cha kuwanyima Wanafunzi chakula cha mchana shuleni ni ukatili dhidi ya Watoto; haiwezekani sisi watu wazima tunalazimisha kupata chakula cha mchana halafu watoto wetu hatuwatilii mkazo na tunataka kuona ufaulu unapanda. Hii haiwezekani”. Alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa