Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Agosti 20.2023
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Gairo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Rahel Nyangasi (Diwani Kata ya Chigela) amewahimiza Wazazi kuchangia chakula Cha mchana shuleni ili kuwajengea Wanafunzi tabia ya kupenda shule, bidii ya kujifunza na kuongeza ufaulu.
Ametoa rai hiyo Agosti 14 shule ya Msingi Gairo 'A' wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM ilipofika shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Awali na Msingi ambapo Wajumbe hao walishiriki chakula cha mchana na Wanafunzi hao.
Nyangasi amsesa kitendo cha wazazi kutochangia chakula cha mchana shuleni kwa ajili ya watoto wao ni kitendo cha ukatili kwa watoto na hakikubaliki katika jamii yoyote hivyo kila mzazi anawajibu wa kuhakikisha anashirikiana na Walimu kuchangia chakula cha mchana shuleni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa