Na Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Juni 6. 2024
Ili jamii iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuwezesha Wanafunzi kupata uelewa mzuri darasani, ni lazima kuwepo na uhakika wa chakula na upatikanaji wa lishe bora kwa kuzingatia makundi yote 5 ya chakula.
Kauli hiyo imeelezwa na Mhe. Rahel Nyangasi, Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Gairo, akifungua Kikao cha Kamati ya Lishe Wilaya kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe.Jabiri Makame, kilichofanyika Juni 6. 2024 katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri.
“Changamoto zipo, lakini nmi lazima jamii tushirikiane katika kuhakikisha Changamoto hizi tunazitatua kwa pamoja, kuanzia shuleni kwa wanafunzi hadi watu wazima. Kushinda njaa kutwa nzima bila kupata chochote huwezi kuwa na akili timamu”. Alisema Mhe. Nyangasi.
(MKURUGENZI MTANDAJI WA HALMASHAURI BI. SHARIFA NABALANG'ANYA)
Kikao hicho muhimu cha kujadili utekelezaji wa afua za lishe kimewkautanisha wataalam mbalimbali akiwepo Mkurugenzi wa Halmashsauri, Mganga Mkuu Wilaya, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji, maafisa Kilimo,Mifugo, Uvuvi na Umwagiliaji pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata ambao walisaini Mkataba wa Kutekeleza jukumu hilo baina yao na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Wajumbe wengine ni Maafisa Lishe.
Kupitia hotuba yake Mwenyekiti wa Halmashauri amewataka Maafisa Watendaji wa Kata kufanya ufuatiliaji wa karaibu wa kuhakikisha Wazazi wanachangia chakula kwa ajili ya kuwezesha Wanafunzi kupata chakula cha mchana shuleni sambamba na kusimamiautekelzaji wa sharia ndogo ya Halmashauri ya upatikanaji wa chakula na mlo shuleni.
Kwa upande Mwingine Mhe. Nyagasi ametoa wito kwa Mganga Mkuu Wilaya Dkt. Mahela Njile kupitia Meneja wa Bima ya iCHF kufanya hamasa na elimu kwa jamii wafahamu bima hiyo ya Afya inavyofanya kazi ili wahamasike kujiunga.
Alisema ni muhimu jamii kufahamu njia bora za kupata huduma za afya kwa gharama nafuu, hivyo ni wajibu kwa Wataalam wa Divisheni ya Afya na Ustawi wa Jamii kuandaa utaratibu maalum wa kutoa hamasa kwa wananchi kuhusu Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa iCHF.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa