Na. Cosmas Mathias Njingo.GAIRO
Juni 15.204.
Wito umetolewa kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Itifaki Serikalini kutumia taaluma na nafasi zao katika kuielemisha Jamii kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura, kuhamasisha Wananchi ili washiriki katika zoezi hilo, sambamba na kutoa taarifa sahihi ili kuwawezesha kujua sheria, Kanuni taratibu mbalimbali za kufuata na sifa za wanaostahili kushiriki katika uboreshaji huo.
Wito huo umetolewa Juni 15. 2024 na Mkurugenzi wa Uchaguzi (Katibu) Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania Ndg, Ndg. Ramadhani Kailima, akifungua warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo maafisa Habari, Mawasiliano na Itifaki wa Serikali, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City.
“Tume inatarajia kupata ushirikiano mkubwa zaidi kutoka kwenu, hasa kuhusu zoezi lililopo mbele yetu linalotarajiwa kuanza tarehe moja Julai kuhakikisha mnatoa taarifa sahihi kwa Wananchi na kwa wakati, hasa kuhusu zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga Kura.".
Kailimia amewaambia Maafisa hao kuhakikisha wanashirikiana na Waandishi wa Vyombo vya Habari vya Kijamii vilivyopo katika mikoa na Halmashauri zao, pamoja na kutumia mitandao ya kijamii, ili kufikisha elimu hiyo muhimu kwa Umma sambamba na kukanusha taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi wa viongozi na Wananchi kuhusu zoezi hilo.
“Kumekuwepo na taarifa za upotoshaji kwamba uboreshaji wa Daftari wa Kudumu la Wapiga Kura unahusiana na maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwaka huu 2024. Tumieni nafasi mliyonayo huko kwenye Halmashauri zenu kuujulisha Umma kuwa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, hauhusiani kabisa na maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa”. Alisisitiza Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo wa Tume Huru ya Uchaguzi amewasisitiza Maafisa hao wa Habari kusoma na kuzielewa vizuri Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024, Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Mwaka 2024, Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2024 pamoja na Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapika Kura za Mwaka 2024, ili kutoa majibu na ufafanuzi sahihi kukusu taarifa za wanaopotoshaji.
“Someni vizuri vitabu mlivyopewa vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sheria za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, na vitabu vya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura mtapata mwongozo mpana wa kuwasaidia kutoa taarifa sahihi kukusiana na zoezi la uboreshaji wa taarifa za wapiga kura kwenye Daftari la kudumu”. Alieleza Ndg. Kailima.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimuwa ya Mpiga Kura Bi. Giveness Aswile amesema Wananchi wotewenye sifa ya kupiga kura wataandikishwa katika zoezi hilo hata kama hawana kitambulisho au Namba za Utambulisho wa Taifa (NIDA) pamoja na kuboresha taarifa za Wapiga kura wengine ambao tayari orodha yao ipo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura.
Mkutano huo unahitimisha mfululizo wa mikutano ambayo Tume imefanya na wadau mbalimbali wake kauanzia tarehe 07 Juni, 2024, lengo Ia kuwapa wadau hao taarifa za uwepo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari Ia Kudumu la Wapiga, matumizi ya vifaa vya kiteknolojia na mfumo wa uandikishaji pamoja na na ushiriki wa Wananachi wa Wananchi kwenye vituo vya kuandikishia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa