Na. Cosmas Mathias Njingo
GAIRO, MOROGORO
Oktoba 27.2022
Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuboreash huduma za ugani kwa kuwawezesha maafisa ugani ngazi za vijiji, kupata vitendea kazi, ikiwepo usafiri ili kuwafikia wakulima na wafugaji kwa haraka zaidi.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Omari Makame
Amesema hayo Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, katika hotuba yake ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki la Mkulima Wilayani humo Oktoba 27, 2022, kwenye viwanja vyaSoko la Mahindi Kata ya Ukwamani.
Kutoka kushoto: Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Clement Msulwa, Mwenyekiti wa CCM (W) Ndugu Dastan Mwendi, na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame wakisikiliza maelezo kuhusu matumizi ya viwatilifu vya kuulia wadudu kwenye zao la mahindo kutoka kwa Bw. Peter Kihiyo
“Kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya Kilimo, Serikali imendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha huduma za ugani, ili wakulima walime kwa tija; Serikali imenunua vitendea kazi vya kutosha zikiwepo pikipiki ambazo watagaiwa Maafisa ugani katika vijiji vyote ili wawe na uwezo wa kuwatembea na kuwafikia Wakulima kwa haraka zaidi”. Alisema Mhe. Makame.
Baadhi ya Wananchi Walioshiriki maonesho ya shughuli za kilimo katika Wiki la Mkulima wakisikiliza maelezo kuhusu matumizi sahihi ya Mbegu za mahindi kutoka kwa Mtaalam wa Kilimo wa ASA
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa, vitendea kazi hivyo, vitarahisisha wakulima wengi zaidi kufikiwa kwa muda mfup,i na kupimiwa udongo, kupewa elimu na ushauri juu ya matumizi bora ya pembejeo, mbole za ruzuku na mbegu bora zinazofaa kutumika kulingana na mazingira waliyopo, ili walime kilimo chenye tija na kuzalisha mazo mengi.
Wnakikundi cha kuzalisha mafuta ya Alizeti cha Chinyankala kutoka kata ya Rubeho, wakionyesha bidaa zao wakati wa Maadhimisho ya Wiki la Mkulima Wilayani Gairo
Akaongeza kuwa wakulima wengi wanazalisha kiasi kidogo cha mazao kutokana na kukosa elimu ya kilimo bora na matumizi ya mbegu sahihi wakati wa kupanda; ambapo wanazalisha kati ya gunia tatu (03) hadi sita (06) kwa heka moja, halia ambayo alisema ni kiwango kidogo sana ingilinganishwa na wakulima wanaofuata kanuni bora za kilimo.
“Nimetembelea baadhi ya vijiji na kuzungumza na Wakulima mbalimbali, kila Mkulima niiyemuuliza anapata mazao kiasi gani anasema anazalisha kati ya gunia tatu hadi sita kwa ekari moja. Hii si sawa kabisa; kwa mkulima anayefuata kanuni bora za kilimo, anauhakika wa kuzalisha gunia ishirini au ishirini na tano katika eneo la ukubwa wa ekari moja”. Aliongeza Mhe. Makame.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, akitia saini kwenye daftari la wageni alipo tembelea banda la Maonesho ya uzalishaji wa miche ya nyanya inayozalishwa na mjasiliamali Bi. Raha kutoka Msowero Wilaya ya Kilosa, wakati wa madhimisho ya Wiki la Mkulima.
Sambamba la hilo Mhe. Makame akawasisitiza Wakulima kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea za kupandia na kukuzia ili kuongeza rubuta kwenye undogo kwa lengo la kuwezesha mazao kupata rutuba muhimu ya kusaidia ukuaji wake.
Maadhimisho ya Wiki la Mkulima Wilaya ya Gairo, yalizindiliwa rasmi Oktoba 27.2022, na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Jabiri Omari Makame, ambapo yatafanyika kwa muda a siku tatu hadi Oktoba 30, 2022. Shughuli za maonesho ya bidhaa mbalimbali na teeknolojia za kilimo ziliendelea kufanyika ambapo Wakulima walipata fursa ya kutembelea kwenye mabanda ya wadau wakilimo kujifunza ma kujionea shughuli zinazotekelezwa na Wadau.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, akikagua moja ya zana zinazotengenezwa na Mzalendo, wakati wa maonesho ya Wiki la Mkulima
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa