Na. Cosmas Mathias Njingo
GAIRO, MOROGORO
Oktoba 28.2022
Maafisa ugani ngazi ya Kata na Vijiji wametakiwa kuhakikisha wanatoa elimu kwa Wakulima na kuwahamasisha kujisajili katika daftari la Wakulima ili kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali ikiwepo pembejeo za ruzuku.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Wiki la Mkulima katika kata ya Ukwamani, ikiambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali za Kilimo.
“Maafisa Ugani ngazi ya Vijiji na Kata chini ya Afisa Kilimo wa Halmashauri, hakikisheni mnawafikia Wakulima na kuwapa Elimu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la wakulima kwani serikali inaleta fedha ili kuwawezesha wakulima kunufaika na fursa mbalimbali ikiwepo unafuu wa upatikanaji wa pembejeo na mbolea za ruzuku”. Alisema Mhe. Makame.
Kwa upande Wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Dastan Mwendi aliipongeza Serikali kwa juhudi kubwa inazozifanya katika kuwakomboa wakulima hasa kwa kutenga bajeti kubwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya kuinua sekta ya Kilimo.
“Ndugu zangu Serikali yetu kupitia Wizara ya Kilimo kwa mwaka huu wa fedha imetenga bajeti kubwa haijawahi kutokea, lengo ni kuhakikisha sekta ya kilimo inainuka na kuwafanya wakulima kupata tija katika uzalishaji. Naipongeza sana Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kipaumbele katika sekta ya Kilimo.
Naye Diwani wa Kata ya Gairo na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Danistan Mwegoha, alisema maonesho hayo ya Wiki ya Mkulima ni fursa pekee kwa wakulima kujifunza mbinu na kanuni bora za kilimo sambamba na kujionea teknolojia mbambali zinazoweza kumwinua mkulima na kuboresha uzalishaji wa mazao.
“Ninawasihi wakulima kuyatumia vizuri maadhimisho haya ya wiki la Mkulima maana kuna elimu mbalimbali zinatolewa, hii itawasaidia Wananchi kujifunza na kupata uelewa mzuri kuhusu kanuni bora za kilimo cha kisasa sambamba na ufugaji wenye tija”. Alisema Mhe. Mwegoha.
Baadhi ya Taaisi za Kifedha zikiwepo Bank ya CRDB, EQUITY na NMB zimesema zipo tayari kuwakopesha wakulima mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha kujikwamua kwa kufanya kilimo bora cha kisasa chenye tija.
Wawakilishi wa Taasisi hizo za kifedha zimedai kuwa zinamuwezesha mkulima kupata Mkopo wa Tekta, fedha taslimu kwa ajili ya kusaidia gharama za kilimo kuanzia usafishaji wa shamba, upatikanaji wa mbegu, mbolea na shughuli zote za shamba hadi kufikia
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa