• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Authorities Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira
    • Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni za Halmashauri
      • Seksheni ya Rasilimali Watu
      • Seksheni ya Utawala
    • Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Baraza la Madiwani
  • Miradi
    • Miradi ya Maendeleo
      • Sekta ya Elimu Msingi
        • Miradi Mipya
        • Miradi iliyokamilika
      • Sekta ya Elimu Sekondari
      • Sekta ya Afya
      • Sekta ya Barabara/Miundombinu
      • Sekta ya Maji
  • Machapisho
    • Katiba ya JMT
    • Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
    • Hotuba Mbalimbali
    • Sera ya Elimu
    • Taarifa za Hesabu za Mwisho
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MAAJABU YA TASAF KUWAONDOA WANANCHI KATIKA HALI YA UMASKINI

Posted on: October 7th, 2022

Na. Cosmas Mathias Njingo.

GAIRO, Morogoro.

Tarehe 7. Oktoba 2022

Katika jitihada za Serikali za kufanikisha lengo namba moja kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs), la kutokomeza umaskini, Tanzania ilianzisha mfuko wa Taifa wa Maendelo ya Jamii uitwao TASAF ukiwa na lengo la kuzinusuru kaya Maskini zaidi Nchini.

Bi. Elis Alexanda AZILIKAMU ni miongoni mwa wanufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya maskini Zaidi (TASAF) ambaye kwa sasa anasema maisha yake yamebadilika kwa kiasi kubwa na kupiga hatua kiuchumi.

“Maisha niliyonayo leo ni maisha yatofauti mno nayale niliyokuwa ninaishi kabla ya kuja huu mpango wa TASAF, na kutusaidi sisi wanawake tuliotelekezwa na Wanaume zetu na kutuachia watoto kuwalea wenyewe. Sina wasiwasi tena juu ya matunzo na malezi ya Wanangu maana TASAF inatulea vizuri”. Alisema Bi Azilikamu, alipotembelewa n Mwandishi wetu”. Alitamba Bi. Azilikamu.

Elis A. Azilikamu, mnufaika wa Mpamgo wa Kunusulu Kaya Maskini Zaidi-TASAF, akihudumia mbuzi aliowapata kupitia mpango huo baada ya kuwekeza fedha kidogo kidogo katika kibubu (Picha Na, Cosmas M. Njingo-GAIRO)

Bi. Azilikamu anaeleza kuwa siku aliyoitwa kwenda ofisi za Kata kupokea fedha zake kwa mara ya kwanza hakuamini wala hakupata usingizi kwani, swala la kupata pesa bila kufanya kazi yoyote kwa dunia ya leo haliwezekani, lakini kwa Serikali ya Tanzania limewezekana kupitia Mpango wa Kunusuru kaya Maskini TASAF.

“Ujue siku ya kwanza tuliitwa ofisi za kata kwa ajili ya kupokea fedha, kwanzan nilijua ni uongo tu pengine kuna jambo linguine tulikuwa tunaitiwa kule, Niliogopa sana. Lakini baaya ya kuambiwa nisaini hati ya malipo ya fedha kiasi cha Shilingi elfu Arobaini, nilihisi kuvhanganyikiwa kwa furaha niliyokuwa nayo. Nahapo ndiyo nikaamini maajabu ya TASAF katika kutuondoa kwenye umaskini sisi wenye kipato cha chini”.  Alifafanua mnufaika huyo.

Bi. Azilikamu ni Mama wa Watoto 5, kati ya hao 3 wanajishughulisha na shughuli za kilimo cha bustani ya mbogamboga baada ya kuhitimu darasala saba, mmoja amehitimu elimu ya msingi mwaka huu anasubiri matokeo kujiunga na kidato cha kwanza 2023, na mdogo wa mwisho ana umri wa miaka 4, ambaye anatarajiwa kuanza elimu ya awali ifikapo 2023.

Mnufaika huyo anasimilia kuwa, baada ya kupokea fedha za mpango wa kunusuru Kaya Maskini kwa mara ya kwanza kiasi cha Tsh.40, 000 (elfu arobaini) alianzisha kilimo cha mbogamboga, shughuli anayo endelea nayo hadi sasa ambayo ilimuwezesha kuanza kununua mbuzi kidogo kidogo.

“Lianza kulima busta, nikuza mboga pesa nyingine ninahifadhi kwenye kibobo nyingine natumia kwa matumizi mbalimbali ya kujikimu na mahitaji ya chakula na madaftari ya watoto ambao kwa wakati huo walikuwa bado wanasoma, baadaye nilipofungua Kibobo zilikuwa zimefika 41,000 nikanunua mbuzi jike mmoja”. Alisema.

Muonekana wa nyumba ya Bi.Azilikamu aliyokuwa akiishi hapo awali kabla ya kuingia kwenye mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF
(Picha Na. Cosmas M. Njingo-GAIRO)

Nyumba ya pili amayoishi kwa sasa yeye na familia yake, aliyoijenga baada ya kuanza kupokea ruzuku kutoka TASAF, aliyoijenga kutokana na kilimo cha mbogamboga (Picha Na. Cosmas M. Njingo)

Hivi sasa Bi. Azilikamu anamiliki mbuzi wapato 18 wenye thamani ya zaidi ya Sh. 1,000,000 ambapo anasema kupitia shughuli ya ufugaji wa mbuzi ameweza kujenga nyumba bora yenye vyumba vitatu na sebule ambayo anatarajia kuhamia hivi karibuni baada ya kukamilika kwa ujenzi wake.

Muonekano wa nyumba mpya ya vyumba 3 na sebule ya Bi. Azilikamu, anayoijenga kwa fedha za ufugaji wa Mbuzi. Tayari mbao zipo za kupaulia zimekamilika, anajumla ya bati 20 bado bati 6 ili kazi ya kupaua ianze (Picha Na. Cosmas M. Njingo).

Bi Elis Alexanda Azilikamu anaipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kusaidia Watanzania Maskini hususani Wanawake Wajane, na ambao walitelekezewa familia na waume zao, halia ambayo anasena maisha yao yalikuwa duni kufuatia kutokana na ukosefu wa uhakika wa kupata shughuli za kujipatia vipato.

Kuhusu ushauri kwa jamii, Bi. Azilikamu amewataka Wanawake wenzake wanaonufaika na mpango huu kujifunza utamaduni wa kutunza fedha kwa lengo la kupata mtaji utakao wawezesha kutimiza malengo na mataraji ya Serikali ya kuwaondoa wanawake kutoka kwenye hali ya umaskini kwa kutumia kiasi kidogo cha fedha wanazozipata kuwekeza kwenye shughuli za kiuchumi.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUITWA KWEYE USAILI WAOMBAJI NAFASI ZA AJIRA MTENDAJI WA KIJIJI III NA DEREVA II September 21, 2024
  • TANGAZO LA HALMASHAURI KUKUSANYA USHURU WA USAFI May 07, 2024
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA PROGRAM YA BBT May 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA DEREVA July 12, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MKOA WA MOROGORO WAJIPANGA KUIWEKA WILAYA YA GAIRO KWENYE RAMANI YA UZALISHAJI WA PARACHICHI NCHINI

    February 19, 2025
  • BARAZA LA WAFANYAKAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA GAIRO LARIDHIA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 18, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, KILIMO NA MIFUGO YAHIMIZA UHARAKISHWAJI WA UJENZI WA BARABARA YA GAIRO-NONGWE

    February 17, 2025
  • KAMATI YA BUNGE YAHIMIZA WAKULIMA VIJIJI VYA MASENGE, MKOBWE KUPADA MITI

    February 15, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAFUNZI DARASA LA SABA WAASWA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • GAIRO ONLINE TV
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255 787730665

    Simu ya Kiganjani: +255 717222572

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa