• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Authorities Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira
    • Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni za Halmashauri
      • Seksheni ya Rasilimali Watu
      • Seksheni ya Utawala
    • Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Baraza la Madiwani
  • Miradi
    • Miradi ya Maendeleo
      • Sekta ya Elimu Msingi
        • Miradi Mipya
        • Miradi iliyokamilika
      • Sekta ya Elimu Sekondari
      • Sekta ya Afya
      • Sekta ya Barabara/Miundombinu
      • Sekta ya Maji
  • Machapisho
    • Katiba ya JMT
    • Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
    • Hotuba Mbalimbali
    • Sera ya Elimu
    • Taarifa za Hesabu za Mwisho
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MADEREVA KUACHA KUBUGHUDHI ABIRIA, KUFUATA SHERIA

Posted on: November 23rd, 2022


Cosmas Mathias Njingo; 

MOROGORO.

Nov 23.2022.

Viongozi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani wamewataka madereva wa mabasi ya masafa marefu kufuata Sheria ili kuepusha ajali katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara (LATRA) Bw. Johansen Kahatano na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani SACP Ramadhani Ng’anzi Novemba 23, 2022 walipokutana katika Ofisi za LATRA Mkoa wa Dar es Salaam na kujadili namna bora ya kudhibiti mwendokasi wa mabasi ya masafa marefu kuelekea msimu wa mwisho mwaka.

Aidha, Bw. Kahatano aliwaasa wadau wa sekta ya usafiri ardhini nchini hasa wasafirishaji, madereva, makondakta na mawakala wanaokata tiketi kuzingatia Sheria na kuitii bila shuruti, “sisi hatutakuwa na muhali na mtu yeyote na atakayekiuka Sheria atakumbana na mkono wa Sheria, kwahiyo nawasihi kuwa kila mdau atimize wajibu wake.”

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi ca Usalama Barabarani SACP Ramadhani Ng’anzi alisema kuwa Jeshi hilo limejipanga vizuri kuhakikisha kwamba wale wanaokiuka sheria za usalama barabarani wanachukuliwa hatua bila kuoneana aibu, “Tuna imani kuwa madereva ambao wana leseni na wamepitia katika vyuo vya mafunzo ya udereva watafuata kanuni zinazowaongoza barabarani, sisi kama Jeshi la Polisi hatutosita kuchukua hatua stahiki kwa yeyote atakayebainika anavunja Sheria ya Usalama Barabarani.”

“Tunashukuru wenzetu wa LATRA wameanzisha mfumo wa tiketi mtandao ambao umesaidia sana kudhibiti wale wanaozidisha nauli kiholela na hivyo nawasihi wale wanaokata tiketi wazikate kwa njia ya mtandao. Kwa madereva nawasihi wafuate kanuni na alama zinazowaelekeza barabarani vinginevyo wasije wakatulaumu," alisisitiza SACP Ng'anzi.

LATRA na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabara wanafanya kazi kwa ukaribu kuhakikisha kwamba kunakuwa na udhibiti katika sekta ya usafiri ardhini na hasa katika kuhakikisha kuwa suala la ajali linapungua nchini.

Matangazo ya Kawaida

  • Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za Gairo December 16, 2022
  • SOMA TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KADA MBALIMBALI May 25, 2022
  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUZOA TAKA, KUFANYA USAFI NA KUKUSANYA USHURU WA USAFI June 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 19, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YATAKA UFANISI KATIKA UFUATILIAJI WA MAREJESHO YA MIKOPO YA ASILIMIA 10

    December 07, 2022
  • WAGANGA WAKUU, WAFAMASIA WA HALMASHAURI WAHIMIZWA KUZINGATIA TARATIBU ZA UTOAJI DAWA

    December 06, 2022
  • SHERIA NDOGO YA KUDHIBITI SUMUKUVU KUWABANA WAKULIMA, WAUZAJI, WASAMBAZAJI, WASINDIKAJI WA MAZAO.

    December 05, 2022
  • WANAOISHI NA ULEMAVU, WAASWA KUTOJITENGA NA JAMII INAYOWAZUNGUKA

    December 03, 2022
  • Tazama zote

Video

VIBE LA MAKARANI WA SENSA GAIRO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • GAIRO ONLINE TV
  • MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA SITA 2022 GAIRO SEKONDARI
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255232935454

    Simu ya Kiganjani: +255 767498981

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa