Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, limemuomba Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini-TARURA kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuwabana Wakandarasi wanaopewa kandarasi za ujenzi wa mabarabara, kuhakikisha wanalipa ushuru wa huduma (service levy) ili kuiwezesha Halmashauri kukusanya mapato ya ndani kupitia chanzo hichon kwa lengo kufikia makusanyo ya shilingi 23,549,234,374 iliyojiwekea katika mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Mhe. Rachel Nyangasi pamoja na Kaimu Mkurugunzi wa Halmashauri Bi. Susan Nyanda wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha Kupitia, kujadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya TARURA Wilaya ya Gairo kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mjadala wa kikao hicho Mhe. Nyangasi alimwambia Meneja wa Tarura Saimon Masala kuwa Halmashauri inapoteza fedha nyingi za ushuru wa huduma kutokana na usimamizi mbovu kwa wakandarasi hali ambayo inachangia Wakandarasi hao kutoroka na mapato ya serikali.
“Namimi ninaungana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri kukuomba Meneja wa TARURA kusaidia katika eneo hili la kukusanya ushuru wa Huduma kwa wakandarasi wote unaowapa kazi ya ujenzi wa mabarabara ya hapa Gairo”, aliomba Mhe. Nyangasi.
Akaongeza “Ushuru huu mkiusimamia vizuri Halmashauri itaweza kukusanya vizuri lakini pia itatuwezesha Waheshimiwa Madiwani kujua kwenye Mpango wa Bajeti zetu za kila mwaka tunakusanya kiasi gani kutokana na ushuru wa huduma unaopaswa kulipwa na Wakandarasi”, alibainisha Mwneyekiti huyo.
Mhe. Nyangasi akafafanua zaidi kuwa kumekuwepo na hali ya uzembe katika kufuatilia na ukusanyaji wa ushuru wa huduma kwa wakandarasi,na kuongeza kuwa hali hiyo inawanyima wananchi kunufaika na uboreshaji wa miundo mbinu ya huduma mbalimbali za kijamii kutokana na kupotea kwa fedha ambazo zingeweza kutumika katika kuwaletea maendeleo kupitia miradi mbalimbali.
“Fedha zinazo potea ni nyingi zingeweza kuwanufaisha wananchi kupitia miradi ya maendeleo ambayo Halmashauri inapanga kutekeleza kila mwaka, lakini inashindwa kutokana na ukusanyaji hafifu wa mapatao hususani kwenye eneo hili la ushuru wa huduma za kandarasi mbalimbali za ujenzi wa miundombinu ya mabarabara”, alisistiza Mhe. Nyangasi.
Akimkaribisha Mwenyekiti kufungua Kikao hicho Maalum cha Baraza la Madiwani Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Susan Nyanda alimuomba Meneja wa TARURA kushirikiana kwa pamoja katika kusimamia ukusanyaji wa ushuru huo kwa kuweka mikakati ya pamoja ya ili kuepusha utoroshwaji wa mapato kutoka kwa wakandarasi hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa