Na. Cosmas Mathias Njingo. Gairo
Mei 30. 2024
Wahe.Madiwani wameaswa kuwasimamia na kushirikiana na Maafisa Watendaji wa Kata katika zoezi la ukusanyaji mapato pamoja na kusikia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliikamilike kwa wakati na katika ubora uliokusudiwa.
Rai hiyo imetolewa na Mhe. Ramadhani Kimwaga, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri (Diwani Kata ya Chakwale) akifungua Mkutano wa Baraza la Wahe.Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za maendeleo ya Kata kwa robo ya III katika kipindi cha Januari-Machi 2023/2024, uliofanyika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri Mei 23.2024.
"Wahe.Madiwani niwaombe twende tukasimamie ukusanyaji wa mapato kwa kushirikiana bega kwa bega na Watendaje wa Kata. Pia tukahakikishe tunasimamia kwa karibu utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo hasa Ujenzi wa miradi mbalimbali ili ikamilike kwa wakati na katika ubora na viwango vilivyowekwa". Alisema Mhe. Kimwaga.
Diwani huyo akizungumza Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rachel Nyangasi, ambaye alichelewa kufika kwenye mkutano huoo kwa kazi Maalum, aliwaambia Wahe.Madiwani hao kuwa swala la Ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa Miradi ya Maendeleo siyo jambo la Watendaji wa Kata peke yao,bali linamhusu moja kwa moja Diwani wa Kata husika, hivyo ni vyema kushirikiana Kwa pamoja ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuwafikia Wananchi na kuwapa huduma zilizo Bora.
Aidha Makamu Mwenyekiti huyo aliipongeza ofisi ya Mkurugenzi, Timu ya Wataalam wa Halmashauri ambayo inaundwa na Wakuu wa Divisheni na Vitengo, pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata, kwa kusimamia na kutekeleza Maazimio ya Wah. Madiwani waliyoyatoa katika Vikao vilivyopita yakiwataka kuweka mikakati madhubuti ya kusimamia makusanyo ya mapato ya Serikali.
Kwa upande mwingine Mhe. Kimwaga aliwasisitiza Viongozi hao kuongeza usimamizi na kuhakikisha mazao ya biashara hayatoroshwi na Wafanyabiashara wasiowaaminifu ambao wamekuwa wakitorosha mazao kwa nia kuiibia Serikli.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa