Juni 1.2023
Watumishi wa Ajira Mpya Kada mbali mbali walioripoti Halmashsuri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, wametakiwa kufanya kazi kwa bidii, kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma sambamba na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatatisha ajira zao.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Utumishi kutoka Divisheni ya Utawala na Rasimali Watu, Bi. Jane Sanga, wakati wa kikao elekezi kwa watumishi hao, kilichofanyika Mei 29.2023 katika ukumbi mdogo wa Mikutano wa Halmashsuri.
"Kwa hiyo, kila mmoja wenu, anatakiwa kuhakikisha anatekeleza wajibu wake kikamilifu kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu pamoja na kuzingatia taraibu na kanuni za Utumishi wa Umma, pia ni muhimu sana kwa Watumishi wa Umma kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kusababisha kufukuzwa kazi", alisisitiza Bi. Sanga.
Kwa Upande wake Afisa Tawala Bw. Given William aliwaambia watumishi hao kuzingatia Waraka wa Utumishi Na. 6, wa mwaka 2020 kuhusu Mavazi kwa Watumishi wa Umma unaolekeza aina ya Mavazi yanayotakiwa kuvaliwa na Watumishi wa Umma.
"Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 6, wa mwaka 2020 kuhusu Mavazi kwa Watukishi wa Umma unataja bayana aina ya Mavazi yanayotakiwa kuvaliwa na Watumishi wa Umma, lakini pia umeweka makatazo kadha ya aina za nguo ambazo Watumishi wa Umma hawaruhusiwi kuvaa kwenye maeneo ya kazi". Alisema Bw. William.
Afisa Tawala huyo akaongeza kusema "Waraka huu pia umekataza wazi wazi kwa wanawake kuweka rangi kwenye nywele 'yaani brich' na kuchora tattoo. Aidha hairuhusiwi kwa Wanaume kutoga masikio na kuvaa hereni". Alisistiza.
Naye Afisa Tawala II Divisheni ya Utawala na Rasimali Watu Bw. Abuu Liwangira aliwambia Watumishi hao kujenga nidhamu ya kazi na utii, kuwahi kazini kwa muda uliopangwa sambamba na kutoa huduma pasipo upendeleo kwa misingi ya itikadi ya vyama, kabila au dini.
"Tambueni kuwa wajibu wetu ni kutoa huduma kwa watu wote bila upendeleo kwa misingi ya Ukanda au Ukabila, Dini au Itikadi ya chama flani ya cha Siasa Tunatakiwa kuwahudumia Wananchi wote, hii ndio maana ya Utumishi wa Umma". Alisistiza.
Mafunzo hayo yalijumuisha Watumishi Kada ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Mhandisi Ujenzi, Fedha, Manunuzi,Utawala na Usafirishaji
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa