Wakuu wa Shule za Sekondari na Maafisa Elimu kata wamepewa mafunzo ya kujengewa uwezo juu ya matumizi ya Mfumo wa Takwimu shule za Sekondari (SIS), lengo ikiwa ni kupata uelewa wa pamoja wa ukusanyaji na uingizaji wa takwimu sahihi katik mfumo huo
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Bi. Tatu Mkango, amewataka Walimu wakuu shule za Msingi na Wakuu wa Shule za Sekondari kushirikiana na Maafisa Elimu kata, kuhakikisha shule zote Wilayani Gairo zinakuwa na Masanduku mawili ya maoni (sanduku la furaha na Sanduku la huzuni), ili kurahisisha ukusanyaji wa takwimu za vitendo vya ukatili dhidi ya watoto
ametoa wito huo Machi 28.2023 wakati wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa ukusanyaji Takwimu shule za Sekondari (SIS) yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa