Mwenge wa Uhuru 2022, ukiwa Wilayani Gairo, ilikimbizwa katika maeneo mbalimbali, ambapo uliona, kuzindua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi 6,yenye thamani ya Sh.Bilioni 1,198,476,916.72.
(Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omary Makame akipokea Mwenge wa Uhuru, kutoka kwa Mkimbiza Mwenge Kitaifa)
Agosti 24.2022 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabiri Omari Makame, alipokea Mwenge wa Uhuru Kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatuma Mwasa, ambaye aliupokea Kimkoa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamula, kisha kukimbizwa katika Tarafa ya Gairo, kupita kwenye vijiji 11 kati ya 50 na kufika kwenye miradi 6.
(Wakimbiza Mwenge Kitaifa, wakati wa Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2022)
“Mhe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, katika kutekeleza wa Maudhui ya Mwenge wa Uhuru 2022, utapita katika Tarafa 1 kati ya 2, kata 11 kati ya 18, vijiji 11 kati ya 50, ambapo utapitia miradi 6”. Alisema Mhe. Makame.
Akaongeza kuwa “Katika miradi hiyo 6, Mhe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ipo itayoonwa, kuzinduliwa ma kuwekewa mawe ya Msingi. Miradi hiyo imegharimu jumla ya shilingi 1,198,476,916.72”. Alifafanua.
Miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2022 ni pamoja na Mradi wa Vijana watengeneza Majiko katika Kitongoji cha Kwawalesha, Kata ya Ukwamani wenye thamani ya Sh 21, 439,680, kati ya hizo Sh. 15,000,000 zilizotokana na 4% sehemu ya Mkopo wa 10% kwa Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.
Utazindua Mradi wa ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa shule ya Sekondari Majembwe, wenye thamani ya Tsh.78, 312,830.72, Utaweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharula (EMD) wenye thamani ya Tsh.259, 184,378.00.
(Mradi wa Ujenzi wa Barabra ya Msingisi Guest-Ramashop (Manyara), kwa fedha za tozo)
Miradi mingine itakayo wekewa Mawe ya msingi ni Mradi wa ujenzi wa Barabara ya Ramashop-Msingisi (Barabara ya Manyara) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami wenye thamani ya sh. 247,637,790.00 fedha za Tozo ya miamala ya simu, na Mradi wa Kituo cha kuuzia mafuta (MC Petro Station), wenye thamani ya Sh.318, 000,000.
(Jengo la Wagonjwa wa Dharura-EMD hospitali ya Wilaya ya Gairo)
Pia Mwenge wa Uhuru 2022 utaweka Jiwe la Msingi katika Upanuzi wa Mradi wa Maji Makuyu kwenda Kinyolisi na Iyogwe, wenye thamani ya sh. 288, 336, 896.95, kisha utafuatiwa na Mkesha wa Mwenge wa Uhuru kwenye Viwanja vya Gairo ‘A’ shule ya Msingi.
(Mradi wa Kituo cha Kuuzia Mafuta (petro station) cga MC)
Aidha ukamilishaji wa miradi hiyo, umechangiwa na fedha za michango kutoka Serikalini Kuu na wadau mbalimbali wa maendeleo. Ambapo Serikali Kuu imetoa kiasi cha Shilingi 856,423,771.05, Mchango wa Halmashauri Shilingi. 16, 377, 239.00, Watu Binafsi Shilingi 318,000,000 na Mchango wa Mwenge Shilingi 1,000,000, na kufanya jumla kuu ya Fedha za michango ywa mwenye kuwa shilingi 1,198,476,916.72.
(Moja ya Mradi uliopitiwa na kuwekewa jiwe la Msingi na Mbio za Mwenge wa uhuru 2022, upanuzi wa Mradi wa Maji kati ya Kinyorisi, Makuyu hadi Iyogwe)
Mwenge wa Uhuru 2022 ulikabidhiwa Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogor Agosti 25,2022
(Shamra shamra za Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kati ya Wilaya ya Gairo na Kilosa)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa