Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Ahmed Shabiby, amewataka wakazi wa Wilaya ya Gairo hususani Vijana, kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao wenyewe sambamba na kutumia vizuri fursa za mikopo inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri.
Ametoa Rai hiyo Oktoba 30.2023 alipokuwa akihutubia Wananchi wa Kata ya Kibedya ambapo pia aligawa mitungi ya gesi kwa Kikundi cha Wauza Maziwa pamoja na Mama Lishe ikiwa ni Kampeni ya kuzuia ukataji wa miti kwa ajili ya kupata nishati ya Mkaa na Kuni.
"Vijane fanyeni kazi kwa bidii, maendeleo hayaji kwa kukaa vijiweni kupiga stories au kucheza pool table na kinywa cooker". Aliwaasa.
Kwa upande mwingine Mhe. Sabiby alitoa Kadi za Pikipiki kwa Kikundi cha Vijana Maafisa Usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kutumia Pikipiki maarufu 'bodaboda' cha HUWILA baada ya kukamilisha marejesho ya mkopo huo wa pikipiki 10 zilizotolewa na Halmashauri kupitia 10% ya Mapato ya Ndani kwa ajili ya Vikundi vya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.
Mbali na hayo pi Mbunge huyo aligawa mipira kwa timu mbalimbali zilizoshiriki kwenye ligi ya Mbunge na Diwani na kuahidi kuziwezesha timu zote kupata mwalimu Bora atakayezinoa tayari kukabiliana na michuano mbalimbali ya soka ya Ndani na Nje ya Wilaya ya Gairo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa