Na. Cosmas Njingo, GAIRO
JANUARI 22.2023
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa, amesema swala la upatikanaji wa Chakula cha Mchana shuleni kwa ajili ya Wanafunzi ni la Wazazi wote kuhakikisha wanatekeleza jambo hilo, nakuwataka walimu kufundisha muda wa masaa ya ziada ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
Mhe. Mwassa alisema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu kilichoambatana na utoaji wa Tuzo ya Kiongozi wa Elimu katika Ukumbi wa Nazareth Wilaya ya Gairo Februari 18.2023.
“Tunaenda kupambana na kuhakikisha Wazazi wanachangia watoto wale chakula cha mchana shuleni, hili ni tatizo kubwa kuliko yote, ni lazima watoto wapate chakula cha mchana shuleni. Hii itasaidia kuongeza ufaulu na kupunguza utoro”. Alisema Mhe. Mwassa.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro alisisitiza kuwa ili kuongeza ufalu kwa watoto ni lazima chakula cha mchana kipatikane kwa uhakika na kwamba uwekwe utaratibu mzuri wa kuhakikisha wanapata kufundishwa muda wa ziada pamoja na kuongeza maonbezi ili kuwajengea uwezo watoto wa kupata mbinu za kujibu mitihani.
“Wakisoma muda tu ule uliowekwa hautioshi, hivyo ni lazima wasome muda wa ziada, kwa utaratibu huu ufaulu wao utaongezeka. Lakini pia kuwepo na majaribio ya kila wiki na kila mwezi na pale inapowezekana tushindanishe shule moja na nyingine”. Alieleza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa