Upanuzi wa Mradi wa maji kwa ajili ya kumhudumia Vijiji vya Magenge na Ndogomi. Mradi huu utagharimu kiasi cha Sh.550,123,571.08 za Mfuko wa (NWF).
Kwa mujibu wa taarifa ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini-RUWASA Gairo, Mradi unahusisha ujenzi wa tenki lenye ukubwa wa lita za ujazo 150,000 juu ya ardhi, na tenki la kuhifadhi maji kwa muda mfupi (Sump Tank) chini ya ardhi lenye ukubwa wa lita za ujazo 75,000.
Shughuli nyingine ni uchimbaji wa mitaro ya kulazia mabomba, kuunga bomba kwa mfumo wa fission na viungio, kulaza na kufukia mbomba urefu wa km 23.9 pamoja na ujenzi wa vituo (DP) vya kuchotea maji Vijiji vya Magenge na Ndogomi.
Kukamilika kwa mradi huu kutapunguza adha ya maji kwa wakazi wa Vijiji hivyo na kuwaondolea kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Aidha Wananchi 7,610 watanufaika na Mradi huu utaboresha utoaji wa huduma kwa Jamii na kuchochea ukuaji wa maendeleo kwa kasi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa