Na. Cosmas Mathias Njingo;GAIRO
Mei 31.2023
Serikali haiwezi kufadhili miradi yote ya mendeleo Nchi nzima kwa kutegemea Fedha za mapato yake ya ndani, hivyo imebuni utaratibu mpya wa kutafuta Fedha nje ya bajeti kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ya Kimkakati.
Kaimu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Mipango na Uratibu Mkoa wa Morogoro Ndg. Anza-amen Ndossa amesema ili kupata Fedha za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Kimkakati nje ya Bajeti Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imeandaa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo Maafisa Mipango, Wachumi, Wataalam wa Ujenzi na Maafisa Biashara, Viwanda na Uwekezaji.
Amesema kwa Mkoa wa Morogoro tayari umeanza kutekeleza mpango huo wa kutoa mafunzo elekezi kwa Wataalam hao ili kuwajengea uwezo wa kupata mbinu na njia bora za uandishi wa maandiko ya miradi mbalimbali ya Kimkakati
"Serikali ikaja na njia mbadala kwa ajili ya kutafuta Fedha nje ya bajeti yake ya kawaida. Sasa ili kupata Fedha hizo kuna namna ya kuandika maandiko. Na sisi tumeona ni vyema tukawajengea uwezo Wachumi wetu wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro" alisema Bw. Ndossa.
Kwa Mkoa wa Morogoro mafunzo hayo yanafanyika kwa siku Nne kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo chini na uwezeshaji wa Maafisa kutoka Idara ya Mipango na Uratibu Ofisi ya Rais TAMISEMI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa