Na. Cosmas m. Njingo
MOROGORO
Agosti 1. 2023
Imeelezwa kuwa; Pamba, Katani na Kahawa ni miongoni mwa mazao ya kikimkakati yenye faida kubwa kiuchumi kwa wakulima na Taifa kwa ujumla endapo yatatiliwa msisitizo ili kuongeza uzalisha na tija kwa Wakulima.
Mkuu wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima alisema hayo Julai 31.2023 wakati akifanya ziara ya kukagua mabanda mbalimbali ya Halmashauri zinazoshiriki Katika Maonesho ya shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi; maarufu nane nane ili kujionea maandalizi ya maonesho hayo ya Kanda ya Mashariki 2023, katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Manispaa ya Morogoro.
“Sisi Mkoa wa Morogorg shabaha yetu ni kuhakikisha Pamba, Katani na Kahawa yanafufuliwa, huu ni mkakati madhubuti wa kuinua uchumi wa mkulima mmoja mmoja na Mkoa kwa ujumla, kwani mazao haya yakiimarishwa uzalishaji wake yataleta tija kubwa kwenye kuongeza kipato cha Mkoa wa Morogoro kutonana na makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri kuwa juu”. Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Malima amesema Mkoa kutokanan na umuhimu wa mazo hayo katika kuinua pato la Taifa kupitia sekta ya kilimo, Mkoa wa Morogoro unalenga kufufua mazao hayo na kuyafanya kuwa mazao ya kimkakati mbayo awali yalikuwa yakizalishwa kwa wingi katika Mkoa wa Morogoro.
Akiwa katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Mvomero VOMERO Mhe. Mhe. Malima amelisema imefika wakati Halmashauri za Mkoa wa Morogoro ziwekeze kwenye kilimo cha mazao hayo na kwamba Kilimo cha Pamba, Katani na Kahawa ni chanzo kizuri na kikubwa cha mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mhe. Malima akabainisha kuwa miche ipatayo milioni moja ya zao la Kahawa inatarajiwa kutatolewa na Taasisi ya Utafiti wa Mbegu Bora za Kilimo (TaCRI), na kwa kuanzia miche hiyo itapandwa katika Halmashauri za Mvomero na Morogoro na baadae zoezi hilo kuendelea katika halmashauri nyingine za Mkuoa huo.
Aidha Mhe. Malima, amezitaka Halmashauri kuhakikisha zinahamasisha wakulima kulima mazao yenye mchango katika mapato yao, jhuku akitolea mfano wa Halmashauri ya Kilosa ambayo imekusanya zaidi ya shilingi milioni 220 kupitia zao la maharage pekee.
Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro, aliambatana na Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Tanga na Dar es Salaam ambayo inaunda Kanda ya Mashariki, ili kujionea maandalizi ya maonesho ya nanenane ambayo hufunguliwa Agosti 1 kila mwaka huku yakiambatana na jumbe za kuhamaisha shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuwa endelevu.
Kwa Mwaka huu, Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanabebwa na kaulimbiu isemayo “Wanawake na Vijana ni Msingi endelevu wa Chakula”, huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Mhe. Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Serikali ya awamu ya Nne.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa