Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Juni 6. 2024Maafisa Watendaji wa Kata Wilaya ya Gairo wametakiwa kutoa elimu na hamasa kwa Umma na kusimamia Wananchi kushiriki zoezi la usafi wa mazingira kila jumamosi ya mwisho wa juma badala ya kuwaachia Viongozi wa Serikali kufagia kwenye maeneo yao, ili kuweka mji katika mazingira safi na nadhifu.
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Sharifa Nabalang’anya akichangia hija mbalimbali katika kikao cha Kamati ya Lishe Wilaya cha kupitia taarifa za utekelezaji wa Afua za Lishe kwa Robo ya Tatu y kipindi cha Januari-Machi 2023/2024, kilichofanyika Juni 6. 2024 kwenye Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri.
“Gairo yetu ni chafu sana, hapa hapa mjini lakini hata ukitembelea kata za pembezoni nako hali ya usafi haipo vizuri takataka zimezagaa. Tuhakikishe tunasimamia maswala ya usafi, nmeshatoa maelekezo ya maandishi kwa Watendaji wote wa kata kwamba kuanzia tarehe 1 Juni 2024, swala la usafi lifanyika kila jumamosi ya kila wiki’. Alielekeza Bi. Nabalang’anya.
Mkurugenzi huyo alisema kila mwananchi mahala alipo anawajibika kuhakikisha anafanya usafi wa mazingira yake na kuhakikisha anahifadhi taka kwenye vyombo maaluma vya kuhifadhia taka au kusizusanya kwenye maeneo yaliyotengwa aili kurahisisha shughuli za uondoaji wa taka hizo pindi gari inapopita kwa ajili ya kutekeleza zoezi hilo.
Aidha Nabalang’anya alisema kumekuwepo na tabia isiyo faa ya Wananchi kuwaachia Viongozi Waandamizi ndani ya Wilaya, Wakuu wa Taasisi na Watumishi wa Umma kufanya usafi kwenye maeneo ya Wananchi huku wao wakijifungia ndani kusubiri muda wa zoezi la usafi usihe ndio wajitokeze kufungua biashara zao.
“Gairo inashangaza sana, yaani siku za usafi wa mwisho wa mwezi wanaojitokeza kufanya usafi ni Viongozi na Watumishi tena wanawafanyia usafi wananchi wakati huo wenye maeneo maeneo yao wamejifungia ndani kusubiri muda wa kufungua maduka ufike ndiyo watoke, hii ni sawa. Haipendezi usafi wa mazingira uwe unafanywa na Watumishi”. Alisema
Alisema kuwa Timu ambazo zitakuwepo zikiongozwa na Watendaji wa Kata, zihakikishe zinatoa elimu kwa Wananchi na kuwasimamia washiriki kufanya usafi wao wenyewe kwenye maeneo yao kila mwisho wa wiki.
"Haipendezi Viongozi wa Serikali wanaenda kufagia mbele ya duka la Mwananchi. Hilo ni eneo lake anafanya biashara kwa manufaa yake na familia na familia yake, halafu amwachie kiongozi amfanyie usafi. Tunapozungumza Lishe na Afya hatuwezi kuacha kuhimiza maswala ya usafi wa mazingira”. Alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Bi. Nabalang’anga akatilia mkazo Zaidi katika kata 3 za mjini ikiwepo Magoweko, Gairo na Ukwamani ambazo ndiyo zimebeba taswira nzima ya Mji wa Gairo, na kwamba maeneo mengi ya kata hizo hususani barabara Kuu ya Morogoro Dodoma yanakabiliwa na takataka nyingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa