Na. Cosmas Mathias Njingo, GAIRO
Julai 2.2023
(Ujenzi wa vyumba 3 vya Madarasa na matundu 3 ya Vyoo shule ya Msingi Chinyankala Kata ya Rubeho)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Bi. Sharifa Nabalang'anya amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali Sekta ya Elimu Awali na Msingi kupitia fedha za BOOST.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Juni 30.2023 kwenye kata za Rubeho, Ukwamani, Gairo, Magoweko, Mkalama na Leshata, Mkurugenzi huyo ameridhishwa na hatua mbalimbali za Ujenzi zilizofikiwa na kupongeza juhudi zinazofanyika licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa kwa baadhi ya maeneo ikiwepo changamoto ya upatikanani wa maji.
(Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Gairo 'A' yenye jumla ya vyumba 14 Elimu Msingi, Vyumba 2 vya Madarasa ya Awali na Matundu 18 ya vyoo)
Akitoa maelekezo ya Jumla, Bi. Nabalang'anya amewataka Walimu Wakuu wa Shule za Awali na Msingi na Wajumbe wa Kamati za Ujenzi kwenye Shule zote zinazotekeleza Ujenzi wa Miundombinu kwa fedha za BOOST, kuimarisha usimamizi na kuongeza ufanisi ili miradi hiyo ikamilike katika ubora wake hasa hatua za umaliziaji wa majengo hayo."Nawapongeza sana wote mmefanya kazi nzuri ingawa natambua kwamba zipo changamoto kadha wakadha katika utekelezaji wa miradi hii. Lakini kikubwa kuliko yote ni Ubora wa Miradi hii. Ni lazima umaliziaje wake uwe katika Ubora wa hali nya juu hasa kwenye upigaji wa plasta na koplo za madirisha" . Alisisitiza Mkurugenzi huyo.
(Ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarasa Shule ya Msingi Kitaita kata ya Leshata)
Bi. Nabalang'anya akatumia fursa hiyo kuelekeza kuwa shughuli za ujenzi ziende sambamba na zoezi la upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira hasa katika maeneo ambayo hayana changamoto kubwa ya maji.Kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo amewaagiza Walimu Wakuu wa Shule hizo kihakikisha wanaongeza kasi ya Ujenzi ikiwezeka kazi zifanyike usiku, hivyo maeneo ya utekelezaji wa miradi hiyo yawekewe taa zenye mwanga wa kutosha ili kuwawezesha mafundi kufanya kazi usiku kwa lengo la kufikia muda uliopangwa wa kukabidhi Miradi hiyo.
(Ujenzi wa Nyumba ya Walimu 2/1, pamoja na Vyimba 2 vya Madarasa ya Shule ya Awali Shule ya Msingi Leshata)
Pamoja naye, Mkurugenzi Nabalang'anya aliambatana na Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Msingi Mwl. Emma Kobona, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji Bi. Msifwahi Haule, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ndg. Cosmas Njingo, pamoja na Mhandisi Ujenzi kutoka Divisheni ya Miundombinu Mijini na Vijijini.
(Ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarsa Shule ya Msingi Lukungu Kata ya Ukwamani)
(Ujenzi wa Matundu 3 ya vyoo na Vyumba 3 vya Madarasa Shule ya Msingi Majawanga Kata ya Mkalama)
(Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa ya Awali, Vyumba14 vya Madarasa ya Shiule ya Msingi na matundu 18 ya Vyoo Yeriko Kata ya Magoweko)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa