Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Japhari Kubecha, amefanya kikao na watumishi wa kilimo wa wilaya hiyo ili kujadili hatua za kuboresha sekta ya kilimo na kuimarisha maendeleo ya kilimo katika eneo hilo. Kikao hicho kilijumuisha mapitio ya mkakati wa ukuaji wa kilimo, huku pia kikijikita katika maandalizi ya tamasha la “Samia Kilimo Expo”, litakalofanyika hivi karibuni.
Katika kikao hicho, Kubecha alisisitiza umuhimu wa wadau kushirikiana na wilaya ili kuhakikisha maonesho hayo yanafanikiwa kwa kishindo. Tamasha hilo linalenga kuonesha fursa mbalimbali za kilimo, kujifunza mbinu mpya za kilimo, na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau na wananchi. Wadau wa kilimo wanakaribishwa kushiriki maonesho haya ili kuunga mkono maendeleo ya kilimo katika Wilaya ya Gairo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa