Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini Tanzania imewaagiza vyama vya siasa vilivyothibitisha kushiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kuwasilisha taarifa za gharama za uchaguzi.
Hii inahusisha gharama za maandalizi, kampeni, na siku ya uchaguzi.
Wito huu umetolewa na Bi. Edna Esey, afisa kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa Tanzania bara, akiambatana na Bi. Ummy Gumbo kutoka ofisi ya Msajili Visiwani Zanzibar.
Bi. Esey ametoa wito huo katika kikao na viongozi wa vyama vya siasa kilichofanyika Septemba 7, 2025, kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
Esey ametaja sababu za kuwasilisha gharama hizo kuwa ni pamoja na:
kuongeza
1.Uwazi na Uwajibikaji: Kuwa na taarifa sahihi za gharama kutasaidia katika kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa vyama vya siasa.
2.Mpango wa Fedha: Taarifa hizo zitasaidia pia katika kupanga na kudhibiti matumizi ya fedha wakati wa kampeni, smbamba na kuweka bayana pamato na matumizi ya fedha za chama ikiwepo michango mbalimbali kutoka kwa washirika na wadau wao
3.Sheria na Kanuni: Ni muhimu kwa vyama kufuata sheria na kanuni za uchaguzi zinazohitaji kuwapo kwa ripoti za gharama hizo.
4.Kukuza Demokrasia: Kupitia uwazi wa gharama, demokrasia itaimarishwa na wananchi wataweza kufanya maamuzi bora wakati wa uchaguzi.
Amesema hatua hiyo ni muhimu kuelekea uchaguzi mkuu, ambayo inakumbusha vyama vya siasa wajibu wao wa kutoa taarifa sahihi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa