PICHA 1: Diwani wa Kata ya Kibedya Mhe. Butindi Massatu (mwenye koti la kijani) kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dakta Godbless Luhunga wakati wa makabidhiano ya pikipiki 10 kwa kikundi cha HUWILA cha bodaboda kutoka kata ya Kibedya
Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Kikundi cha Vijana wa waendesha pikipiki za kusafiirisha abiria (Boda boda) HUWILA kilichopo kata ya Kibedya Wilaya ya Gairo, kimepokea mkopo unaotokana na 10% ikiwa ni sehemu ya makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri ambazo hurudishwa kwa jamii ili kunufaisha vikundi vya kiuchumi vya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.
PICHA 2: Diwani wa Kata ya Magoweko Mhe. Ibrahimu Mmbwana wakati wa makabidhiano ya pipiki 10 za mkopo kwa vijana wa kikundi cha HUWILA zenye thamani ya Ths. 26 milioni.
Kikundi hicho cheye vijana 10 (Me 9 na Ke.1) Kimekabidhiwa jumla ya Pikipiki 10 zenye thamani ya Shilingi 26,000,000 (Milioni ishirini na Sita) ambazo ni 4% zinazoelekezwa kwa Makundi ya Vijana, wakati Wanawake hupewa 4% huku Watu wenye Ulemavu wakipata 2% na kufanya jumla ya mkopo wote kwa makundi hayo kufikia 10%.
Akikabidhi Pikipiki hizo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rachel Nyangasi, Diwani wa Kata ya Magoweko Mhe. Ibrahimu Mmbwana amewataka Vijana hao kuwa waangalifu na kuzitunza pikipiki ziho ili ziwe na manufaa kwao na kujikwamua kiuchumi.
Diwani wa kata ya Magoweko Mhe. Ibrahimu Mmbwana akiendesha moja ya pikipikii zilizotolewa mkopo kwa kikundi cha Vijana wa HUWILA sehemu ya 10% za mkopo wa vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu
“Ushauri wangu kwenu ni kuhakikisha mnazitunza vizuri hizi pikipiki ili zilete tija kwanu na kwa familia zenu zinazo wategemea. Mkizitunza nao zitawatunza.” Alishauri Mhe. Diwani Mbwana.
Diwani Mbwana aliwambia Bodaboda hao kujiona wao wana bahati kubwa sa kupata mkopo huo kwa wakati huu kwani vipo vikundi vingine vingi ambavyo vimewasilisha maombi ya kupewa mkopo lakini bado havijafanikisha kutimiziwa azima hiyo hivyo ni muhimu kwao kuvilinda vyommbo hivyo sambamba na kulipa mkopo ili kuwezesha vikundi vingine kunufaika na fursa hiyo.
“Msidhani mpo peke yenu wenye sifa za kupata hizi pikipiki, ninyi mna bahati kubwa sana, kwani hata mimi katani kwangu kuna vikundi vingi vimewasilisha maombi Halmashauri ya kupewa Mkopo lakini bado havijafanikiwa, ninaimani mkirejesha kwa wakati pesa za mkopo huu mtawezesha na wengine kupata mkopo hivyo mhakikishe mnakuwa waaminifu katika kurejesha kila mwezi.” Alisistiza.
Naye Diwani wa Kata ya Kibedya Mhe. Butindi Massatu ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha vijana hao kupitia mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri na kuahidi kuwafatilia ili warejeshe mkopo huo kwa wakati uliopangwa.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. Godbless Luhunga amewaasa vijana hao kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuhatarisha usalama wa maisha yao na pikipiki hizo.
Akimkaribisha Nhe. Diwani Ibrahimu kukabidhi pikipiki hizo kwa kikundi cha HUWILA kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri Bi. Rachel Nyangasi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauiri Dakta. Godless Luhunga aliwambiwa vijana hao kuhakikisha wanalinda usalama wa maisha yao na vyombo hivyo kwa kujiepusha na ajali za barabarani.
“Serikali inawapenda ndiyo maana imewaletea pikipiki hizi, lakini mara zote mkumbuke kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kujihakikishia usalama wa Maisha yenu na vyombo hivi mlivyo pewa ili visilete hasara kwa familia zenu ambazo zinawategemea kwa kiasi kikubwa. Nimuhimu sana kutii sheria bila shuruti, na msiache kuvaa kofia ngumu wakati wote muwapo kazini. Alisema Dakta Luhunga.
Awali Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii (W) Ndg. George Katoto aliwambia Bodaboda hao kukahikishi wanahifadhi pesa kwenye akaunti yao ya kikundi kila wiki na kuwasilisha nakala za malipo hayo kwa Mhasibu wa Kikundi ili kuingiza kwenye daftari la kumbukumbu na kwamba kila mwisho wa mwezi fedha hizo ziwekwe kwenye akaunti ya Halmashauri ikiwa ni marejesho ya kila mwezi ya Mkopo huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa