Mwalimu Mstaafu Mama Lesso amewaasa Wanafunzi wa Shule za Msingi na sekondari kutonyamaza pindi wanapokumbana na vitendo vya ukatili wa kijisia sambamba na kuheshimu mila na desturi za Kitanzania.
Akiongea na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rubeho katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Wiki ya Wanawake. Mama Lesso alisema Watoto wa Kike wanakabilia wa changamoto mbalimbali ikiwepo vitendo vya ukatili lakini wanakaa kimya kutokana na baadhi ya familia kuendekeza mfumo dume na mila potofu hali inayozima ndoto za watoto wa kike kutimia.
Kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani mwka 2023 ni āUbunifu na Mabadiliko ya Teknolojia,Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia.. ambapo maadhimisho ya kilele cha siku hiyo yabatarajiwa kufanyika Machi 8.2023 katika viwanja vya Gairo A Shule ya Msingi huku mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Mhe. Fatuma Mwassa, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
HakimilikiĀ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa