Aprili 21.2024
Na., Cosmas Njng.o GAIRO
Wilaya ya Gairo imepokea na kuanza rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, mapokezi hayo yamefanyika katika viwanja vya Tabu Hoteli Kata ya Chigela, ukitokea Wilaya ya Mvomrro, ambapo unatarajiwa kukimbizwa katika Tarafa ya Gairo umbali wa Kilometa 176.30
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa kichocheo kikubwa cha kuimarisha Amani, upendo, Umoja na Mshikamano, pamoja na kuhamasisha na kuharakisha Maendeleo katika Wilaya ya Gairo. Kwa mwaka huu miradi 9 itafikiwa na Mbio za Mwenge Uhuru yenye thamani ya Shilingi 1,594,217,370.12, ikiwepo nguvu za Wananchi shilingi 209,518,293.79, Halmashauri ya Wilaya Shilingi 25,083,310.00, Serikali Kuu Shilingi 759,096,907.00, Wahisani Shilingi 588,733,359.30 na Mfuko wa Jimbo Shilingi 11,785,500.00
Aidha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 zitafanya shughuli mbalimbali Wilayani Gairo katika Miradi ya maendeleo ikiwepo uwekaji wa Mawe ya Msingi katika miradi 3, Kufungua miradi 2, Kuzindua miradi 2 na Kuona miradi 2. Miradi hiyo ni ya Sekta za Afya, Maji, Kilimo, Malisili na Mazingira, Elimu, Uwezeshaji Wananchi kiuchumi/Maendeleo Jamii, Utawala Bora, Barabara, Huduma za Jamii na Mapambano dhidi ya Rushwa.
Mwenge wa Uhuru ni Chombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika. Mnamo mwaka 1964 Mwenge wa Uhuru ulianza rasmi Mbio zake, baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliounda Nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 ni “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa