Mhe. Rachel Nyangasi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, ametoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vilivyopo sambamba na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuiwezesha Halmashauri kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwepo uendeshaji wa Halmashauri hiyo.
Ametoa rai hiyo Wilayani Gairo wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani cha uwasilishaji, kupokea na kupitia Taarifa za kila kata za utekelezaji wa shughuli za maendeleo, katika kipindi cha robo ya nne cha Januari Machi 2021, kilichofanyika Juni 9 2021 katika ukmbi wa mikutano wa Halmashauri.
“Swala la ukusanyaji mapato lipo ndani ya uwezo wenu, ni wajibu wa kila Mheshimiwa Diwani kusimamia kikamilifu makusanyo yanayotokana na vyanzo vilivyopo, lakini pia ni vyema kuwepo na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato katika kata zenu”. Alisema.
Mhe. Nyangasi ambaye pia ni Diwani wa kata ya Chigela alisisitiza swala la kuimarisha ushirikiano baina ya Waheshimiwa Madiwani na Watendaji waandamizi wa Halmashauri pamoja na watenda wote kuanzia ngazi za vijiji hadi kata, katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, upangaji wa matumizi sambamba na utekekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti Nyangasi alisema “Maendeleo hupatikana kwa kasi kwenye jamii inayojitambua na yenye kushirikiana vizuri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na Sisi Waheshimiwa madiwani tukumbuke kushirikiana vizuri na wataalamu wetu wa Halmashauri, pia tushirikiane na watendaji kuanzia ngazi za vijiji hadi kata tunazoziongoza ili Wananchi waone faida ya kutuamini na kutupigia kura katika uchaguzi uliopita ili tukapiganie maslahi yao”.
Akabainisha kuwa kumekuwepo na sintofahamu kwa Madiwani hao kupelekewa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeeo kwenye kata zao pasipo kupewa taarifa, hali ambayo alisema inarudisha nyuma kasi ya ukuaji wa maendele kwa kuto kushirikishwa kuanzia mwanzo hivyo kusababisha kushindwa kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha husika, ambapo alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kusimamia jambo hilo.
“Naagiza Mkurugenzi hii sintofahamu sasa iishe, inawezekana vipi kupeleka fedha za mradi kwenye kata bila kumpa taarifa Mwenyekiti wa Maendeleo ya Kata ambaye ni Diwani wa kata husika?” Mhe. Mwenyekiti alihoji.
Kwa upande mwingine Mhe. Nyangasi amewataka walezi wa kata kufika kwenye kata zaowalizo pangiwa kuzihudumia kwa ajili ya kukagua, kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu kwenye utakelezaji wa shughuli mbali mbali za maendele zinazotekelezwa ili kuongeza kasi katika ufuatiliaji pamoja na kuchochea ukusanyaji wa mapato.
Hata hivyo kikao hicho kili ahirishwa baada ya Waheshimiwa Madiwani kutoridhishwa na taarifa za mapato na kubaini kuwepo na dosari wakati wa kuandaa taarifa hizo, ambapo Madiwani hao walimuomba Mwenyekiti wa Halmashauri kusitisha kikao hicho na kutoa muda kwa Mweka Hazina kandaa upya taarifa iendane na taarifa za kata na zile zinazozalishwa na mfumo wa kukusanya mapatao
Kikao cha Baraza la Madiwani cha kupokea, kujadili na kupitisha taarifa za maendela ya kata kiliahirishwa, ambapo Mwenyekiti Nyangasi alitaja kuwa kitafanyika tena Juni 15 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa