Na. Cosmas Njingo, GAIRO
JANUARI 20.2023
Mwalimu Nassibu Abdalla wa shule ya sekondari Rubeho amejinyakulia kitita cha Fedha sh. 500,000. (Laki Tano) kwa kufaulisha vizuri somo la KISWAHILI.
Kamati ya maandalizi ya sherehe za kilele cha Wiki ya Elimu ilimzawadia fedha Taslimu Sh.450,000 (Laki nne na Elfu Hamsini) hali ambayo ilimfurahisha Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro Mama Germana Mng’oha na kuongeza kiasi sh.50,000 (hamsini elfu) hivyo kujinyakulia kiasi hicho cha fedha.
Kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo, shule ya sekondari rubeho imeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya Taifa ya Mitihani ya Kidato cha Pili na yakuhitimu Kidato cha Nne ikiwa na wastani wa daraja D kwa masomo; mage bila sifuri hali ambayo imechangia vijana wengi wanaohitimu shuleni hapo kupata fursa ya kuchaguliwa kuendelea na elimu ya Juu ya Sekodari (Advanced Certificate of Secondary Education-ACSE) pamoja na vyuo vya kati ikiwepo vyuo vya ualimu.Baadhi ya Walimu wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame kwa kuanziasha utaratibu wa kuadhimisha Wiki ya Elimu na kuongeza kuwa utaratibu huo utaleta hamasa kwa walimu na kuongeza ari ya kufundisha na kujifunza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa