Na. Cosmas Mathias Njigo. GAIRO
Juni 6.2024
Wito umetolewa kwa Watendaji wa kata kufanya hamasa na kutoa elimu kwa Wananchi watambue umuhimu wa kujiunga katika Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa iCHF, sambamba na kuongeza kasi ya uandikishaji wa Wanachama wa mfuko huo ili kuwezesha Wananchi wengi kupata huduma za Afya kwa gharama nafuu.
Wito huo umetolea na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame, akizungumza na Watendaji wa Kata pamoja na wajumbe wa Kamati ya Lishe Wilaya, katika kikao cha Kamati hiyo cha kupitia na kujadilia taarifa za utekelezaji wa afua za Lishe kwa robo ya tatu kipindi cha Januari Machi 2023/2024, kilichofanyika kwenye Ukumbi Mkubwa wa Mikutanao wa Halmashauri Juni 6. 2024.
“Hapa sasa nguvu ya ziada inahitajika, nendeni mkatoe elimu kwa Wananchi kuhusu Bima ya iCHF na kuwahamsisha wajiunge kwa wingi, pia ongezeni kasi kasi ya uandikishaji kwenye vijiji vyote ili Wananchi wajiunge wapate uhakika wa huduma za afya kwa gharama nafuu wakati wowote wanapohitaji kutibiwa”. Alielekeza Mhe. Makame.
Awali Meneja wa iCHF Wilaya ya Gairo Bi. Joanitha Mashasi aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa mojawapo ya changamoto zinazokwamisha zoezi la uandikishaji ngazi za vijiji ni ukosefu Maafisa Waandikishaji wenye uwezo na wanaomiliki simu janja, pamoja naufinyu wa bajeti kununu vitendea kazi hususani Simu janja ambazo zinatumia mfumo wa IMIS kwajili ya uandikishaji na ukusanyaji wa michango ya Wateja.
“Mhe. Mweyekiti Mfumo huu mpya wa iCHF unatakiwa kutekelezwa kwa kutumia simu janja ambazo kimsingi Halmashauri inatakiwa kuzinunua na kuzigawa kwa Maafisa Waandikishaji ngazi za Vijiji, lakini ufinyu wa bajeti umekwamisha kupata simu za kutosha kugawa katika vijiji vyote 53”. Alisema bi Mashasi
Mratibu huyo akaongeza kuwa juhuzi mbalimbali zimefanyika ili kukabiliana na changamoto hiyo kwa kipindi cha mpito, ambapo alitaja kwamba ni kutumia baadhi ya Wahudumu wa Afya waliotayari kutekeleza zoezi hilo kwa kutumia simu zao kufanya uandikishaji katika vituo vya kutolea huduma za afya ngazi za Zahanai, Vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya.
“Changamoto ya ukosefu wa rasilimali watu na vifaa imetufanya kubuni mbinu ya kuwaomba baadhi ya watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya kufanya uandikishaji kwa kutumia simu zao ambazo zimewekewa mfumo wa iCHF, baada ya kuwahamasisha na kuwapa mafunzo ili wasaidie kutekeleza zoezi hilo kwenye vituo vya vya huduma za afya.” Alifafanua Meneje huyo.
Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe. Makame amewaagiza Watendaji hao kuanza mchakato wa kuwapata Wananchi ambao wanamiliki Simu janja na ambao wapo tayari kufanya kazi ya uandikishaji wa Wananchi wanaojiunga katika Bima ya iCHF kwani ni sehemu ya kujipatia kipato pia kuongeza idadi ya Wananchama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa