Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Julai 24.2023
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. @jabiri_makame_ Makame akiambatana na Katibu Tawala Wilaya, Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi Afande Mhina Donati pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri @sharifa_nabal wamefanya ziara kukagua shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu katika mgodi Mpya ulioibuliwa na wachimbaji wadogo wadogo Kata ya Leshata.
Katika ziara hiyo @jabiri_makame_ Makame na Viongozi wenzake wamebaini kuwepo kwa changamoto kadhaa mgoni hapo
1.usalama hafifu kutokana na ukosefu wa vifaa maalum vya kujikinga na majanga hafifu kwa kusokena vifaa maalumu vya kujikinga ma majanga. 2.Wachimbaji kukosa Leseni na uhalali wa kuendesha shughuli hiyo.
3.Kuwepo kwa Watoto wadogo chini ya Mika 18 eneo la mgodi badala ya kwenda shule.
4.Utoroshwaji wa mapato ya Halmashauri na
5.Ufuatiliaji na usimamizi hafifu wa Afisa Madini na Maafisa mapato.
Kufuatia kubaini changamoto hizo Mhe. Makame akapiga marufuku kwa wachimbaji hao kuruhusu watoto kuzagaa kwenye eneo la mgodi, Kuhakikisha madurufu ya Serikali yanakusanywa kikamilifu,Afisa Madini kuhakikisha anatoa elimu ya usalama kwa wachimbaji hao waweze kuchukua tahadhari za kujikinga na majanga mbalimbali; Afisa Madini ahakikishe wachimbaji hao wanajiunga kwenye vikundi na kusajiliwa kwa lengo la kupata leseni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa