Jeshi la Polisi Wilaya ya Gairo, limewataka watoto wanaoishi katika mazingira magumu kuishi kwa upendom kujiepusha na dhambi, sambamba na kutoa taarifa dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya kikatili pamoja na kuwafichua wahusika wa matukio hayo.
Hayo yamesemwa Machi 7.2023 na Viongozi Waandamizi Wanawake wa Jeshi hilo wakati wa ziara yao kutembelea Kituo cha Kulelea Watoto wanaotoka katika mazingira magumu na Yatima cha Betheli, ikiwa ni kuadhimisha Wiki ya Wanawake Duniani kuelekea Kilele cha Maadhimisho yako ambayo Kimkoa yatafanyika Wilaya ya Gairo Machi 8.2023.
Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Gairo SP WEGESA SANJUKILA amewambia watoto hao kuishi kwa kuzingatia mafundisho ya dini wanayoelekwa na viongozi wa ili kuepuka dhambi.
"Wanangu wazuri mimi ninawaomba muishi kwa kufuata mafundisho ya dini kama ambavyo walimu na viongozi wenu wanavyowaelekeza ili kuimarisha upendo, umoja na mshikamano". Alisema SP SANJUKILA
Mkuu wa Dawati la Jinsia Wilaya wa Jeshi hilo INSP. HOPE TARIMO aliwambia watoto hao kutojiona wanyonge na badala yake wajiamini na kutokubali kudharauliwa na mtu yoyote na kwamba watoe taarifa endapo kuna watu wanataka kuwaonea na kuwatendea vitendo visivyofaa.
"Msikubali mtutu yoyote kuwadharau wala ninyiwenyewe msidharau watu wengine. Mnachotakiwa kufanya kwanza na kujiamini, pia msiache kutoa taarifa dhidi ya matukio ya ukatili na manyanyaso mkiona wezetu wanafanyiwa" Alisema Afande Hope.
kwa upande wake #AFISA POLISI JAMII ASP JOYCE KILIMUGISHA aliataka watoto hao kutoa taarifa sahihi kwa watu sahihi bila woga ili kuliwezesha jeshi hilo kukabiliana nawatu wanaojihusisha na matukio ya ukatili dhidi ya Watoto.
"Mnatakiwa kutoa taarifa sahihi, mahali sahihi na kwa watu sahihi ili hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya wahisika badala ya kutoa taarifa kwa watu wasio husika" alisema ASP Kilimugisha.
Pamoja na mambo mengine Jeshi hilo la polisi likiongozwa na wanawake limetoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa watoto waliopo kituoni hapo ili kuwazesha kujikimu pamoja na kusherehekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani.
Askari hao walikabidhi Mbuzi mmoja kwa ajili ya mboga, mchele kilo 20, mafuta ya kula na viburudisho vingine
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa