Cosmas Mathias Njingo;
MOROGORO.
Nov 27.2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza watunza kumbukumbu kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo ya kiutendaji ndani na nje ya Serikali ili kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii wanayo ihudumia pamoja na kuepuka malalamiko mbalimbali.
Mhe. Rais Samia ametoa agizo hilo Novemba 27.2022, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Wanataaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Jijini Arusha (AICC).
“Ni wajibu wenu kuhakikisha mnatekelza majukumu yenu kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu sana, kwa kuzingatia Sera, Sheria, kanuni na Miongozo mbalimbali ya kiutendaji ili kuboresha utoaji wa huduma, na kuondoa malalamiko kutoka kwa Wateja wenu mnao wahudumia”. Aliagiza Mhe. Samia.
Mhe. Rais Samia akaongeza kwa kuwataka Wanataaluma hao wa kutunza kumbukumbu na nyaraka katika ofisi za umma, pamoja na mambo mengine, wanawajibu wa kuhakikisha wanasimamia vyema maadili ya taaluma yao kwa kutunza siri za Serikali, lengo ikiwa ni kuhakikisha nchi inakuwa katika hali tulivu na salama.
“Ninyi ni watu muhimu sana katika Serikali yetu na Taasisi zake zote, hivyo moja ya maadili ya kazi yenu ni utunzaji wa Siri za Serikali. Nendeni mkasimamie vyema maadili ya taaluma yenu, mkihakikisha Siri za Serikali hazivuji vuji hovyo, kuepusha kuleta taharuki kwa Umma, au kuingiza Nchi kwenye machafuko kutokana na ukosefu wa vifua vipana vya kutunza Siri za Serikali”. Alisisitiza Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa awamu ya Sita”.
Kwa upande mwingie Mhe. Rais Samia ametoa wito kwa waajiri Serikalini na Sekta binafsi kuhimiza matumizi ya teknolojia kwenye utunzaji wa kumbukumbu ili kuimarisha mazingira ya kazi kwa kupunguza mrundikano katika vyumba vya masijala.
“Matumizi ya teknolojia katika utunzaji wa kumbukumbu utasaidia kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa haraka pale zinapohitajika k wa ajili ya maamuzi mbalimbali. Na hii itarahisisha sana utoaji wa huduma bora pamoja na kuondoa mrundikano wa majalada vyumba vya Masjala”. Alisisitiza Mhe. Rais.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza watunza kumbukumbu kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa