Na. Cosmas Mathias Njingo, DAR ES SALAAM
Juni 17. 2024
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anatarajwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Kikao cha 19 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Itifaki wa Serikali, ambacho kitatanguliwa na Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari Nchini tarehe 18-19 Juni 2024.
Mbali na Rais Samia, viongozi wengine watakaoshiriki ni pamoja na Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu wa Wizara na Manaibu Katibu Wakuu, Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari Maelezo, baadhi ya Wakuu wa Taasisi za Umma, Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini, Wahariri na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari.
Kikao hicho ambacho kimeratibiwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kinalenga kuwajengea uwezo Maafisa Habari, Mawasiliano na Itifaki hao wa Serikali, kuwaongezea waledi kwa kuwapa mbinu mpya jinsi ya kufikisha taarifa kwa uma kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali ngazi ya Wizara, Taasisi za Umma, Mikoa Majiji na Halmashauri, sambamba na kuongeza ubunifu katika kutekeleza wa majukumu yao ya kila siku.
Kwa mwaka 2024, kikao kazi hicho cha 19 kitafanyika kwa siku 3 kuanzia tarehe 20-24 Juni.2024, huku kikiwa kimebeba Kaulimbiu inayosema "Jenga Mustakabali Endelevu kwenye Sekta ya Habari katika Zama za Kidijiti" ambayo inawakumbusha Wadau wote wa Sekta ya Habari na Mawasiliano kutumia fursa ya Teknolojia katika kuchochea maendeleo na kukuza uchumi kwa kupashana habari zenye tija kwa Umma, sambamba na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inaendeshwa Kidijiti.
Wadau wote wa Sekta ya Habari wanatarajiwa kuungana kwa pamoja katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es salaam, ili kujadili mafanikio, changamoto na mikakati ya kuimarisha na kuboresha Sekta hiyo kwa maslahi mapana ya Taifa, kwa kuzingatia kuwa Sekta ya Habari na Mawasiliano ni Sekta mtambuka inayotegemewa na Wadau mbalimbali na Taifa kwa ujumla, kuleta mabadiliko chanya kiuchumi, kifikra na kijamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa