Na. Cosmas Mathias Njingo
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari kufanya kazi kwa karibu na Serikali katika kutangaza mambo mazuri yanayotekelewa na Serikali kkwa lengo la kuwaletea Wananchi Maendeleo ili kujenga taswira nzuri kwa umma na Uso wa Dunia badala ya kuandika taarifa za kuichafua Serikali na kuleta taharuki kwa jamii.
Ametoa kauli hiyo Juni 19, 2024, akifungua Kongamano la Wadau wa Habari na Mafanikio ya Sekata hiyo mwaka 2024, lililofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City.
“Vyombo vya habari vina wajibu mkubwa wa kutangaza mazuri yanayofanywa na Serikali pamoja na kujenga taswira nzuri ya Nchi yetu katika anga za kimataifa. Tumieni vizuri kalamu zenu kuitangaza Tanzania kwa kuandika habari nzuri badala ya kuandika mabaya na kumtukana Rais.Alisma Rais Samia.
Mhe. Samia alisema kuwa Vyombo vya habari sio mshindani wa Serikali bali ni mdau na mshiriki muhimu katika yanayotendwa na Serikali hivyo, Serikali itaendelea kuweka mifumo mizuri ya Kisera, Kisheria na Kitaasisi, katika kuimarisha uhuru na mazingira ya kazi kwa vyombo vya habari.
“Vyombo vya Habari siyo mshindani wa Serikali. Wanahabari na Vyombo vya Habari ni Wadau na Washirika wakubwa wa Serikali katika kuchochea Maendeleo, kutoa elimu kwa Wananchi, na kutangaza fursa za uwekezaji ndani ya nje ya Nchi, ili kuvutia Wawekezaji kwa lengo la kukuza na kuinua uchumi na pato la Taifa”. AlisisitizaMhe. Rais Samia.
Rais Dkt. Samia amesisititiza Wadau wa Habari hao kufanya uchambuzi wa habari kwa lengo la kupata taarifa sahihi na ushahidi wa kutosha juu ya jambo husika kabla ya kuliripoti kwa Jamii, ili kuwezesha Umma kufahamu uhalisia wa jambo hilo iweze kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.
“Nichukue fursa hii kuwataka Wanahabari na Wamiliki wa vyombo vya habari andika na kuripoti habari zilizofanyiwa uchambuzi wa kina/. Ninaamini kupitiaKongamano hili Wanahabari mliopo mtapokea ujuzi mpya, kujifunza namna ya kutoa taarifa za maendeleo ya kiteknolojia katika sekta za uzalishaji na maendeleo ya jamii”. Alieleza Mhe. Rais.
Alisisitiza kuwa masuala haya ndiyo yanayoifanya Serikali kujenga na kuimarisha uhusiano mwema na vyombo vya habari, hivyo ni wajibu wa Waandishi wa Habari, Wahalili na Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini kulinda heshima ya Serikali pamoja na kuimarisha mashirikiano hayo.
Aidha amewakumbusha wanahabari hao na Wahariri kuhamasisha, kufichua maovu na kutowajibika kunakofanywa na Watumishi na Watendaji wa Serikali wasio waadilifu, sambamba na kutoa mrejesho wa hisia na mitazamo ya Wananchi kwa Serikali yao, na kwmaba hii itasaidia kukuza demokrasia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa