Na Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Julai 1. 2024
Siku chache baada ya Serikali kupitai Wizara ya Kilimio na Umwagiliaji kutangaza rasmi utaratibu mpya wa kununua mahindi kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ambao unatarajiwa kuanza Julai 10.2024. Serikali Wilayani Gairo inapenda kuwasisitiza Wananchi na Wakulima kuhifadhi mahindi ili kuyauza kwa bei nzuri mara baada ya utaratibu huo utakapoanza kutekelezwa.
Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabiri Makame pamoja na Viongozi wengine Waandamizi ngazi ya Wilaya, Chama na Halmashauri, wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa Umma na kuweka Msisitizo kwa Wakulima kutouza Mahindi kwa kupima kwenye madebe au vipimo vilivyo kinyume na Sheria ya Vipimo, na badala yake Mazao yote yapimwe kwa uzito wa kilo kabla ya kuuza au kununua
Elimu hiyo imetolewa wakati wa ziara ya Serikali Nyumbani kwako iliyofanywa na Viongozi hao kwa nyakati tofauti tofauti katika Kata na Vijiji, kwa lengo la kuhamasisha Kilimo cha zao la Parachichi na Tumbaku kibishara, sambamba na kuhimiza Wananchu kuhifadhi chakula ili kusubiri utaratibu wa Serikali wa Kununua Mahindi kupitia NRFA ili kuwaweza wakulima kunufaika na bei.
Aidha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge Mhe. Ahmed Shabiby zinaendelea na mchakato wa kutenga eneo kwa ajili ya kuweka Kituo cha kununulia mahindi katika Wilaya yetu ya Gairo.
Hivyo Wananchi wote mnasisitizwa kuendelea kuwa na subira, kuhifadhi mazao yenu na kufuata maelekezo ya Serikali, wakati Viongozi wakiendelea kukamilisha taratibu mbalimbali za kuwezesha upatikanaji wa Kituo cha kuuzia Mahindi, ili kurahisisha shughuli hiyo ifanyike kwa tija kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NRFA)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa