Na. Cosmas Njingo. GAIRO
Mei 27/2024
Imeelezwa kuwa malengo ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeingia makubaliano na Sekta binafsi ya kuhakikisha inaondoa kero ya Maji kwa Wananchi wa Gairo mradi utakaotekelezwa na pande hizo mbili.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, akifungua warsha ya siku moja ya kutambulisha mpango huo kwa Wadau wa Sekta ya Maji, iliyofanyika Mei 25/2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, ambapo Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa Wilayani Gairo kwa Ubia wa Serikali na Sekta Binafsi,
Makame alisema kuwa ni kuhakikisha inaboresha na kuimarisha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama ni ya uhakika na inapatikana karibu na makazi ya Wananchi.
“Serikali yetu inayoongozwa na Mhe. Dakta Samia Suluhu Hassan inayo nia ya dhati ya kumtua Mama ndoo kichwani kwa kuhaikisha inaboresha na kuimarisha huduma za uhakika za upatikanaji wa maji safi na salamani karibu na makazi ya wananchi”. Alisema Mhe Makame.
Mkuu huyo awa Wilaya akaongeza kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaitaka Serikali kuhakikisha inaondoa kero ya Maji kwa Wananchi ifaikapo 2025, kwa kuhakikisha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama Mijini inafika 95% na 85% upate wa vijijini.
Akitoa Salam za Chama, Mwemyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo Ndg. Danistan Daudi Mwendi, alimpongeza Mhe. Samia Rais wa Jamhuri ya Tanzania kwa kuendelea kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwepo mradi huo wa Maji.
“Nichukue fursa hii kipekee kabisa kutuma salamu zangu za pongezi kwa niaba ya Chama change cha Mapinduzi Wilaya ya Gairo na Wananchi wote wa Gairo, kwa Mhe. Rais Samai kutokana na uchapakazi wake mahiri. Gairo tunaendelea kupokea fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za miradi”. Alisema
Naye Kaimu Katibu wa CCM Wilaya Ngd. Mbarouk Soggo ameipongeza Wizara ya Maji na taasisi zake zote zinashughulika na utekelezaji wa Miradi mbalimbali maji kwa lengo la kuhakikisha Wananchi Wananufaika na huduma bora za upatikanaji wa Maji ya uhakika safi na salama, na kwamba kazi kubwa ya Serikali ni kuhakikisha Wananchi wa mijini na Vijijini wanaondokana kabisa na kero ya ukosefu wa maji safi na salama Wilayani Gairo.
Kwa Upande wake Mweyekiti wa Halmashauri Mhe. Rahel Nyangasi ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya maji Mjini (MORUWASA) kwa kuendesha Warsha hiyo muhimukwa ajili ya kuwajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani an Wadau wengine kuhusu utekelezaji wa Mradi huo wenye ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kwani mafunzo hayo nimuongozo tosha wa elumu kwa Umma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa