Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayo ongozwa na Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza orodha ya majina ya Watumishi wapya Kumi sa Sita Elfu Mia Sita Sabini na Sita (16,676) wa kada za Afya na Elimu huku 261 kati yao ni Watumishi wenye Ulemavu.
Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini OR-TAMISEMI, ajira za mwaka huu zimezingatia vipaumbele mbalimbali ikiwepo waombaji wenye sifa waliotangulia kuhitimu vyuo mbalimbali nchini, Wenye Ulemavu pamoja na umri wa kuzaliwa kwa waombaji wanaokaribia umri wa miaka 45 kuingia katika utumishi wa Umma.
Kapitia takwimu hizo jumla ya Watumishi wapya walio ajiriwa kwa Kada ya Elimu ni 9,800, ambapo Elimu Msingi wapo Watumishi elfu tano (5000) sawa na asilimia 51.02 wakati Elimu Sekondari imepata Waalimu wa Ajira mpya elfu nne mia nane (4,800) sawa na asilimia 48.98, miongoni mwao wakiwepo Walimu wenye Ulemavu kwa Elimu Msingi na Sekondari, na kwamba mgawanyo wa Waajiwa hao wapya umezingatia mahitaji ya Halmashauri jinsi zilivyo walisisha maombi ya uhitaji wa watumshi.
Katika kila Walimu 4 walioajiriwa angalau Walimu 3 wa Elimu Sokondari ni wa Masomo ya Sayansi huku angalau Mwalimu 1 katika kila Walimu 4 walioajiriwa ana Shahada ya Elimu (Ualimu).
ya wakitajwa kufikia 6,876.
Kwa upande wa Afya Serikali imeajiri jumla ya Watumishi 6,876, kati yao Wanawake 3,659 sawa na asilimia 53,21 na Wanaume wanafikia 3,217 sawa na Asilimia 46.79. Aidha Waajiriwa hao katika Kada ya Afya 3,074 ni nafasi ya Muuguzi Daraja la II, Tabibu Daraja la II wapo 1,267 na Daktari (MD) daraja la II wanafika 651. Hata hivyo jumla ya nafasi 736 zimekosa waombaji wenye sifa.
Nafasi zilizo kosa waombaji ni pamoja na Madaktari wa Meno, Mteknolojia wa Mionzi, Tabibu Wasaidizi na Tabibu Meno.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa