Serikali Wilayani Gairo, imepiga marufuku tabia ya baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wenye ulemavu, kwani kwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki zao za msingi ikiwepo kukosa elimu kulingana na uhitaji wao ns wamba tabia hiyo ni unyanyasaji wa kimaumbile.
Marufuku hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Sirieli Mchembe wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika ambayo kiwilaya yamehitimishwa katika kijiji cha Mnyunhe kata ya Kibedya.
“Natoa onyo kali na iwe marufuku kuanzia sasa, mzazi au mlezi yoyote atakayebainika kumficha mtoto wenye ulemavu hatua kali zitachukuliwa dhidi yake, haiwezekani Serikali inahamasisha kila mtoto aende shule halafu wengine wanawaficha watoto wao ndani”, alisisitiza.
Alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaendelea kuboresha miundombinu na kuweka mazingira rafiki kwa walemavu ili kuwawezesha kunufaika na fursa ya elimu bila malipo hivyo jamii haipaswi kuwaficha na kuwa nyanyapaa watoto hao.
Akizungumzia kuhusu swala la wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa masomoni, Mhe. Mchembe aliwambia wazazi kuwa wajitokeze kwenye ofisi za kata kwa jili ya kuandikisha wanafunzi wote waliokatisha masomo kutokana na kupata mimba ili watambulike kisha uandaliwe utaratibu wa kuwarudisha mashuleni kuendelea na masomo.
Aidha aliwaasa wanafunzi wa kike kutofanya mapenzi katika umri mdogo kwani kitendo hicho kinasababisha kupata mimba zisizotarajiwa na kukatisha ndoto zao
Alifafanua “Siyo kwamba serikali imeruhusu mimba mashuleni, hapana lengo ni kuendeleza ndoto za watoto wa kike zilizokuwa zimekatika baada ya kushika ujauzito wakiwa masomoni, cha muhimu watoto wa kike mjitunze na kulinda utu wenu muweze kufikia malengo.
Aidha katika hotuba yake Mhe. Mchembe alisisitiza swala la ushurikiano kati ya wazazi wa walimu katika kufuatilia tabia na mienendo wa wanafunzi pamoja na kuchukua hatua za pamoja dhidi ya wanaume wanaowapa mimba mabinti zao badala ya kumaliza kesi za mimba vichochoroni.
Kauli mbiu ya maadhimishi ya kilele cha siku ya Mtoto wa Afrika mwaka huu ni Tutekeleze Agenda ya 2040 kwa Afrika inayolinda haki za Mtoto
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa