Na Fred Kibano
Chamwino, Dodoma
Disemba 7.2022
Serikali imeagiza kufanyika tathmini ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu ili kubaini kiasi kilichorejeshwa na kuwakopesha wahitaji wengine.
Kauli ya Serikali imetolewa na Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange Naibu Waziri (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI alipofanya ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Chamwino tarehe 06.12.2022 ambapo aliongea na watumishi wa Halmashauri na kutoa maelekezo.
“Fedha zote za mikopo ya asilimia 10 zilizokopeshwa tangu tumeanza mwaka 2018 katika Halmashauri ya Chamwino zijulikane ilikopesha kiasi gani na kiasi gani kimerejeshwa mpaka sasa na kiasi gani hakijarejeshwa, zifanyiwe tathmini ili kujua fedha zinazokopeshwa na zinazorejeshwa” alisema Dkt. Dugange.
Dkt. Dugange ametaka kuwekwa utaratibu maalum kwa kutumia Mfumo uliopo wa mikopo ya asilimia 10 ili kufuatilia kwa ukaribu vikundi vyote viweze kurejesha mikopo kwa wakati na kuwapa fursa wahitaji wengine lengo likiwa ni kuwakwamua vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kiuchumi katika Halmashauri hiyo.
Serikali ilipitisha sheria kwa Mamlaka za Serikali za mitaa nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yao na kuwakopesha vikundi vya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu ili kuwakwamua kiuchumi lakini kuifanya mikopo hiyo kuwa endelevu ambapo tayari imekwishatengenezewa Mfumo wa namna ya utoaji, ufuatiliaji na ufuatiliaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa