Na, Cosmas Mathias Njingo
Gairo, Morogoro
Sepetemba 20.2022
Kwa mwaka wa Fedha 2021/2022, Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ilipokea jumla ya Shilingi Bilioni 2.340 za utekelezaji wa Miradi ya Sekta ya Afya, ambapo kati ya hizo Bilioni 1.450 zilitoka Serikali kuu, Sh. Milioni 500 Fedha za Tozo na Sh. Milioni 390 fedha za Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa,na mapambano dhidi ya UVIKO-19
Utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo mbalimbali Hospitali ya Wilaya, Tsh. 800,000,000 (Picha Na Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Kati ya Fedha hizo Sh. 1.450 zilitolewa na Serikali kuu wa ajili ya uboreshaji wa miundombinu kwenye zahanati za mbalimbali ambapo jumla ya sh. Milioni 300 zilitumika kumalizia mamboma 7 ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi.
Zahanati zilizonufaika na uboreshaji wa miundombinu ya afya na ukamilishaji wa mamboma ni pamoja na Talagwe Shilingi. 50,000,000, Zahanati ya Luhwaji iliyo kata ya Msingisi iliyogharimu kiasi cha shilingi. 50,000,000 na Zahanati ya Tabu Hoteli, Kata ya Chigela iliyogharimu kiasi cha shilingi 50,000,000. Zahanati zote 3 zilitengewa fedha kutoka Serikali kuu kiasi cha Shilingi 150,000,000 kati ya Sh. Bilioni 2.340.
Jengo la Wagonjwa wa nje kituo cha Afya Nongwe, Tsh. 250,000,000 (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Muonekano wa jengo la Wodi ya Wazazi na Upasuaji Kituo cha Afya Nongwe, Tsh. 250,000,000 (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Aidha Shilingi 500,000,000 zilitumika kutekeleza ujenzi wa Kituo cha Afya Iyogwe. Ujenzi huo ulihusisha Jengo la Kuhifadhia Maiti, Wodi ya Wazazi, Upasuaji na nyumba ya Mtumishi kituoni hapo.
Pia katika mchanganuo wa fedha hizo kutoka Serikali kuu, kiasi cha Shilingi 800,000,000 zilitekeleza ujenzi wa Majengo (4) Hospitali ya Wilaya ya Gairo, ikihusisha Jengo la kuhifadhia maiti, Wodi ya upasuaji Wanawake, Wodi ya Upasuaji Wananume na Jengo la Upasuaji Mkubwa.
Jengo la Wodi ya Wagonjwa wa Dharula Hospitali ya Wilaya Tsh.300,000,000 (Picha na Cosmas Mathias Njingo)
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji Bi. Msifwaki Haule, kwenye Kikao cha Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango cha kupitia taarifa za mwezi Julai 2022, Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi 390,000,000 za kutekeleza miradi mbalimbali kwa fedha za UVIKO-19.
Bi. Haule alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Nyumba (pacha tatu) kwa ajili ya Watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo uliogharimu kiasi cha fedha Shilingi 90,000,000 na Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa dharula wenye thamani ya shilingi 300,000,000 na kufanya thamani ya miradi yote iliyotekelezwa kwa fedha za uviko kufikia shilingi 390,000,000.
Ujenzi wa Nyumba ya Watumishi (3/1) hospitali ya Wilaya Tsh.90,000,0000 (Picha na Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Kuhusu miradi ya fedha za Tozo, Bi. Haule alisema, miradi hiyo ilitengewa kiasi cha shilingi 500,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD), Maabara, Kizimba cha kuchomea taka, Jengo la Kufulia, Upasuaji na Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya Nongwe, Tarafa ya Nongwe Wilaya ya Gairo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa