Na cosmas Njingo. MOROGORO
Agosti 2.2023
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetenga zaidi ya shilingi bilioni 900 kwa ajili ya uboreshaji wa Sekta ya Kilimo na Miundombinu ya umwagiliaji, Ubora wa mbegu, upatikanaji wa mbolea, upimaji wa Afya ya udongo na kuongeza Matrekta kwaajili ya kuongeza tija katika Kilimo.
Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu Mustaafu Mhe. Mizengo Peter Pinda Agosti 1.2023 akifungua Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu nanenane kanda ya Mashariki yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Manispaa ya Morogoro.
Alisema, Fedha hizo zitawasaidia Wakulima kulima kilimo chenye tija na kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la Pato la Taifa.
Aidha, Mhe. Pinda pia amezitaka Taasisi za fedha nchini kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa mikopo kwa makundi ya Vijana na Wanawake ili kukuza Sekta ya Kilimo nchini.
Kwa upande mwingine Mhe. Pinda amesikitishwa na hali ya udumavu wa watoto chini ya umri wa miaka 5 ambayo kwa kiasi kikubwa husababishwa na ukosefu wa lishe bora kwa Mama pindi anapokua katika hali ya ujauzito na kuongeza kuwa Mkoa wa Morogoro una tatizo la udumavu kwa 30% ambapo hapo awali ilikua 35%.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa