Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Serikali inaendelea kutekeleza kwa kasi miradi ya maendeleo ya uboreshaji wa miundombinu katika shule za sekondari Nchini, chini ya Programu ya uboreshaji Elimu Sekondari (SEQUIP) ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ilipokea fedha kiasi cha Milioni mia Nne Sabini (Tsh. 470,000,000.00) za Mradi wa ujenzi wa miundombinu katika Shule ya Sekondari Leshata iliyopoa kata ya Leshata Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro.
(Ujenzi wa Jengo la Utawala, shule ya Sekondari Leshata)
Halmashauri ilipokea fedhza hizo Novemba 24. 2021 kupitia Akaunti Na. A/C NAMBA 24010004303 ya Shule ya Sekondari Chakwale iliyopo kata ya Madege, ambapo utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa miundombinu katika Shule ya Sekondari Leshata ulianza rasmi Machi 4.2022.
Utekelezaji wa mradi huu wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari kata ya Leshata unahusisha ujenzi wa jengo la Madarasa Nane, Jengo la Utawala, Majengo ya Maabara za Kemia, Fizikia na Baiolojia, Jengo la Maktaba, Jengo la TEHAMA na Matundu ishirini (20) ya vyoo.
(Ujenzi wa miundombinu ya Madarasa Nane (8) Shule ya Sekondari Leshata)
Hadi sasa mradi wa ujenzi wa miundombinu katika Shule ya Sekondari Leshata umefika kwenye hatua mbalimbali za ujenzi huku baadhi ya majengo yakiwa katika hatua ya upauaji, Upigaji lipu, uwekaji wa fremu za milango na magrili kwenye madirisha na usambazaji wa miundombinu ya nishati ya umeme.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Gairo
Bi. Nivoneia Levery, na taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa shule hiyo Bwana Juma Hamisi Kisairo, kiasi kilichotumika hadi kufikia kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu hiyo ni Shilingi Miloni Mia Nne Laki tatu Sabini na Sita Elfu Mia Sita na Tisa na Senti arobaini na sita tu (403,376,609.46).
“Kwa kweli ujenzi unaendelea vizuri sana, tupo katika hatuia mbalimbali za ukamilishaji wa Mradi huu, hadi sasa tuna salio la Milioni sitini na sita Laki Sita ishirini na Tatu mia Tatu na Tisini na Senti hamsini na nne tu, (66,623,390.54) baada ya kutoa gharama zote za vifaa vya ujenzi na malipo ya mafundi”, alisema Bi. Levery
(Ujenzi wa Jengo la Maabara ya Kemia na Biolojia, shule ya Sekondari Leshata)
Mkuu huyo wa Idara ya Elimu Sekondari alifafanua kuwa kiasi hicho cha fedha kilichosalia kitatumika kukamilisha shughuli za umaliziaji na uboreshaji wa muonekano wa majengo hayo ili kuhakikisha shule hiyo inakuwa katika madhari nzuri ya kuvutia sambamba na kuongeza tahamani ya ubora wa majengo kulingana na thamani ya fedha zilizotolea kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.
“Hadi sasa tumeshatumia kiasi cha shilingi Miloni Mia Nne Laki tatu Sabini na Sita Elfu Mia Sita na Tisa na Senti arobaini na sita (403,376,609.46), tumebakiwa na salio la kutosha kumalizia kazi ndogondogo za uboreshaji wa miundombinu mbalimnali ili kuifanya shule hii iwe katika muonekano nadhifu unaolingana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali yetu”. Alifafanua Afisa Elimu huyo.
Kukamilika kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Leshata kutakuwa ni mwarubaini wa kuondoa utorosho na kuongeza mwamko wa elimu katika kata ya Leshata, kwani wanafunzi wengi waliokuwa wakihitimu elimu ya msingi katani hapo walichaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari kata za mbali kutokana na Kata hiyo kukosa Shule ya Sekondari.
(Ujenzi wa Jengo la Maabara ya Fizikia, Shule ya Sekondari Leshata)
Afisa Elimu Levery akaeleza “Shule ya Sekondari Leshata ni shule mpya, tunatarajia kuifungua rasmi mwakani. Januari 2023 tutapokea Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza kwa mara ya kwanza. Hivyo itachochea ari kupata elimu kwa watoto wa kata hii na itapunguza mimba za utotoni, hasa watoto wa kike ndio wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi njiani wakati wa kwenda na kutoka shule.
Aidha Bi Livery alisema kuwepo kwa Shule hiyo katika kata ya Leshata itapunguza utoro kwani shule ipo karibu, tofauti na awali watoto walisafiri umbali mrefu sana kwenda kata za jirani hali ambayo iliwafanya wengine kukata tamaa na kukatisha masomo.
(Ujenzi wa Jnego la TEHAMA, Shule ya Sekondari Leshata)
Mapema mwezi Januari 2022, ziliundwa kamati mbalimbali ikiwepo kamati ya Ujenzi, Kamati ya manunuzi na Kamati ya Mapokezi na Stoo kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji wa ujezi wa mradi wa miundombinu shule ya sekondari leshata unaenda kasi na katika viwango bora, kwa kuzingatia muongozo uliotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Ambapo Wajumbe wa kamati hizo wanatokana miongoni mwa Wananchi wa Kata ya Leshata.
(Ujenzi wa Matundi 20 ya Vyoo, shule ya Sekondari Leshata)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa