NA Cosmas Njingo. GAIRO
Julai 4.2024
Katika mwaka wa fedha ulioisha wa 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ilipokea na kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 4,574, 453,558.57 za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo sekta za Elimu awali, Msingi na Sekondari pamoja na Afya.
Kwa mujibu wa Mkuruigenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Sharifa Nabalang’anya, kati ya fedha hizo, Sh. 1,377,200,000.00 (Bilioni 1.3) ni fedha kutoka Serikali Kuu, Wahisani Sh. 2,857,669,632.75 (Bilioni 2.8), Mfuko wa Manendeleo ya Jimbo Sh. 69,989,000.00 na Sh. 269,594,925.82 fedha kutoka makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashuri.
Miradi itayotekelezwa kwa Fedha za Wahisani kupitia Mradi wa SEQUIP ni pamoja na ukamilishaji wa Mabweni Sh.100,743,437.35 Shule ya Sekondari Iyogwe Chauya Kata ya Italagwe na Umaliziaji wa Bweni Sh. 45,480, 187.67 Shule ya Sekondari Gairo.
Miradi minigine mipya inayotarajiwa kutekelezwa kwa Fedha za SEQUIP ni ujenzi wa Nyumba 2 (2 kwa 1) kila moja katika shule ya Sekondari Iyogwe Chauya na Chigela ambapo zimetengewa jumla ya Sh. 190 milioni, pamoja na ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya Wanafunzi wa Kidato cha 5 na 6 Shule Sekondari Chigela Sh. 360, 000,000.00.
Pia Halmashauri inatarajia kutumia sh.528, 998, 424.00 kujenga Shule Mpya ya Sekondari ya Kata ya Gairo, ambapo utekelezaji wa ujenzi wa miundomibu ya shule jhiyo unatarajiwa kuanzan hivi karibuni maara baada ya taratibu zote za kifedha na kihandisi kukamilika. Kwa upande wa mapato ya Ndani, Halmashuri iliweza kupeleka jumla ya sh.134, 797,462.91 za mikopo ya 10% ya Wanawake, Vijana na Wenye Mahitaji Maalum, na zaidi ya sh.100 Milioni zilielekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya kijami.
Aidha Bi. Nabalang’anya kwa niaba ya Wananchi wa Halmashauriya Wilaya ya Gairo, amemshukuru Mhe. Dakta Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mahaba ya dhati aliyoonesha kwa Wanagairo kwa kuwaletea Fedha nyingi za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha uliopita 2023/2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa