Kikundi cha Vijana cha wasafirishaji wa abiria na mizigo marufu bodaboda, cha Halmashauri ya zamani (Shabiby Complex) Wilayani Gairo ni moja ya vikundi vilivyonufaika na mkopo wa 10% unaotolewa na halmashauri ukilenga vikundi vya kiuchumi vya Wanawake (4%), Viajana (4%) na Watu wenye Ulemavu (2%).
(mmoja wa waendesha bodaboda kijiwe cha Halmashauri ya zamani Bi. Hellen akiendesha pikipiki aliyokabishiwa)
Kikundi hiki chenye vijana 8 akiwepo 1 wa kike kimepata jumla ya pikipiki 8 zenye thamani ta zaidi ya sh.23 milioni
(Baadhi ya vijana waendesha bodaboda wa kikundi cha Halmashauri ya zamani)
Mapema machi 28.2023 kikundi hicho kilikabidhiwa rasmi pikipiki hizo baada ya kutumiza mashariti yote muhimu ikiwepo Wanakikundi kuwasilisha leseni zao za kuendeshea pikipi, nakala ya Vitambulisho vya Taifa au Namba za NIDA, vyeti vya kuzaliwa na nyaraka nyingine muhimu zilizohitajika kwa mujibu wa kanuni na sheria za mikopo ya 10%.
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha na kuimarisha mikakati ya kuboresha maisha ya wananchi wake kwa kuhakikisha inatekeleza vyema sera ya uwezeshaji wanachi Kiuchumi kupitia vikundi vya uzalishaji mali na kiuchumi katika ngazi za halmashauri kutokana na 10% ya mapato ya ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa